loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Soko la Muhange kunufaisha wananchi wengi Kakonko

SERIKALI Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma imesema soko la mpakani la Muhange ni moja ya miradi ya kimkakati kwao katika kuondokana na umasikini na kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa watu wake wakigusa ongezeko la kipato kwa kaya na mtu mmoja mmoja.

Mkuu wa Wilaya Kakonko, Hosea Ndagala amesema sokoni ni sehemu ya mwisho ya mpango mkakati wa soko hilo na ipo mipango ya uwepo wa soko hilo kuimarisha kilimo na kuongeza uzalishaji kwa kilimo bora.

Ndagala alisema soko hilo litakuwa kituo kikubwa cha kuuzia bidhaa za kilimo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Rwanda na wafanyabiashara wameonesha mwitikio mkubwa kutumia soko hilo.

Ujenzi wa soko hilo ni sehemu ya utekelezaji Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano unaolenga kupunguza uwiano wa idadi ya watu wanaoishi chini ya mstari wa umaskini wa mahitaji muhimu kutoka asilimia 28.2 ya mwaka 2012 hadi asilimia 16.7 mwaka 2020/21 na asilimia 12.7 mwaka 2025/26.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kakonko, Masumbuko Stephano amesem soko hilo ni sehemu ya kitega uchumi ambacho kitasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri.

Stephano alisema pamoja na bidhaa za viwandani, za kilimo ndiyo msingi mkubwa wa soko hilo hasa wakulima wadogo vijijini, wanawake na vijana ili wapate mahali pa uhakika kwa ajili ya soko la mazao yao.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara watakaoendesha soko la Muhange, Justina Amato alisema ujenzi huo ni ukombozi kwao hasa wanawake na vijana ambao kwa muda mrefu walikuwa wakiteseka kwa kukosa mahali palipotulia kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao.

Ujenzi wa soko la Muhange ulitekelezwa kwa gharama ya dola za Marekani 225,000 kupitia UNCDF ambapo serikali kupitia halmashauri ya Wilaya Kakonko ilichangia Sh milioni 170 na utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya lengo la kwanza la malengo ya maendeleo endelevu ambalo linasema ni kufuta umasikini wenye sura zote kila mahali.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi