loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lugola- Vitambulisho vya Taifa ni usalama wa nchi

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema, wakimbizi na raia kutoka nje ya nchi wanapewa vitambulisho vya Taifa hivyo unahitajika umakini mkubwa kwa ajili ya usalama wa nchi.

Waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola amesema leo kuwa, yeyote anayefanya kazi katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) anapaswa kuwa makini na ndiyo maana mamlaka hiyo ipo kwenye wizara hiyo kwa kuwa inafanya kazi za kiusalama.

“Uchakati wa taarifa za mtu binafsi ni suala la kiusalama, tunakwenda nalo kiumakini kuhakikisha kwamba mtu ambaye anatakiwa apewe hiki kitambulisho kwa sababu tunawapa makundi matatu, tunampa mtu ambaye ni raia wa Tanzania, lakini tunampa mkimbizi, lakini pia tunampa mtu ambaye ni kutoka nje ya nchi, tunawapa hivi vitambulisho vitavyoitwa ni vya Taifa”amesema Lugola wakati akizungumza kwenye kipindi cha Asubuhi Hii kinachorushwa na kituo cha redio cha TBC Taifa cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Ameomba Watanzania waelewe kwamba, kuchelewa kupata namba za vitambulisho vya Taifa au vitambulisho vyenyewe si uzembe kwa kuwa kazi hiyo ni nyeti na inahitaji umakini.

“Na ndio maana kuna maneno mawili utambuzi yaani mtu atambuliwe kwanza halafu pia tumsajili halafu ndio tuweze kumhakiki na baadaye ndio tuweze kumpa sasa namba ya utambulisho kwamba huyu tumeridhika nae”amesema Waziri Lugola.

Amesema walipanga hadi Desemba mwaka huu NIDA iwe imesajili watu milioni 24.5 na hadi Novemba 13 takribani Watanzania milioni 20.5 walikuwa wamesajiliwa kwenye mfumo na kati ya hao tayari namba milioni 15.5 zimezalishwa.

“Tunakimbizana kuhakikisha kwamba lengo hilo la milioni 24.5 namba za utambulisho zitakuwa zimekwishazalishwa ifikapo tarehe 31 Desemba kwa hiyo namba zitakuwa zinatumika huku tukiendelea kuhakikisha sasa tunakamilisha kitambulisho chenyewe kiweze kufika kwa kila Mtanzania ambaye amebainishwa na tayari amesajiliwa na taarifa zake binafsi zipo kwenye kanzidata ya Taifa ambayo inamuhusu mwananchi mwenyewe”amesema Lugola.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi