loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walimu 16,000 msingi, sekondari kuajiriwa

WALIMU 16,000 wa shule za msingi na sekondari, wanatarajiwa kuajiriwa hivi karibuni baada ya Serikali Kuu kutoa kibali cha ajira.

Aidha, ajira nyingine zinatarajiwa kutolewa katika sekta ya afya kwa ajili ya watalaamu wa kwenda kufanya kazi katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za wilaya. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitangaza jana bungeni wakati akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Mlalo, Rashidi Shangazi (CCM).

Shangazi aliuliza kuwa “serikali imejenga hospitali za wilaya 69 na vituo vya afya zaidi ya 350, je, ni lini serikali itapeleka watumishi huko na katika sekta ya elimu”. Waziri Mkuu alikiri kumekuwa na uboreshaji mkubwa wa huduma katika sekta hizo mbili, hali ambayo imefanya pia kuwapo na upungufu wa watumishi.

“Wabunge ninyi ni mashahidi wa uboreshaji wa huduma katika ngazi ya kata hadi vitongoji, zahanati katika vijiji na hadi katika hospitali zetu za wilaya nchini kote,” alisema Majaliwa.

Alisema katika elimu, huduma pia zimeboreshwa na hivi sasa kuna utaratibu wa shule bebeshi, hivyo kuongeza mahitaji ya walimu na vifaa katika sekta hizo. Alisema kutokana na hilo, serikali imejipanga kuongeza watumishi kwa kutoa ajira ya vibali kwa sekta hizo mbili pamoja na ile ya kilimo ili watumishi hao waende vijijini.

“Katika mwaka 2016 hadi 2018 tuliajiri walimu elfu sita, na hivi karibuni tutaajiri walimu 16,000 wa sekondari na msingi, tutapunguza uhaba kwa kiasi kikubwa.

“Na pia tutakwenda katika sekta ya afyya kwa ngazi zote hadi wilaya na mikoa. Tutaendelea kuajiri baada ya kupata taarifa, mahitaji. Wito wangu wataalamu hawa zikitangazwa ajira wajitokeze, lakini zaidi wakubali kwenda kufanya kazi kokote walikopangiwa,” alisema Majaliwa.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Mgaya Kingoba, Dodoma

1 Comments

  • avatar
    lucholonga masanga
    04/12/2019

    twasubili hizo ajira za afya ila wafamasia ss mbn hamtuon hasa tulosoma pharmacy council one year course

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi