loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nkamia awalipua ma-RC, ma-DC uhaba wa chakula

MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), amesema kuna maeneo nchini yana upungufu mkubwa wa chakula lakini wakuu wa wilaya na mikoa hawatoi taarifa kwa woga wa kutumbuliwa na Rais John Magufuli.

Ameitaja mikoa ya Dodoma na wilaya zake zote, Singida na Manyara kuwa miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na njaa lakini viongozi wake hawatoi taarifa. Kutokana na hali hiyo, amemwomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, serikali ifanye tathmini ya upungufu huo na kuwapelekea wananchi chakula cha bei nafuu.

“Mikoa hiyo ina tatizo kubwa la upungufu wa chakula lakini viongozi wa kamati za ulinzi na usalama hawatoi taarifa sahihi kwa woga pengine kutokana na kauli ya Rais John Magufuli.”

“Je, serikali ipo tayari kufanya utafiti wa upungufu huo wa chakula na kuwapelekea chakula cha bei nafuu wananchi?” aliuliza Nkamia jana bungeni katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

Akijibu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alikiri baadhi ya maeneo nchini yana upungufu wa chakula uliosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa msimu uliopita. Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi wanapaswa kuratibu hali hiyo kwani serikali inacho chombo chake, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kinachotunza chakula na kuuza kwa bei nafuu kwa wananchi wenye upungufu. Alisema wakuu wa wilaya na mikoa wanapaswa kupeleka taarifa katika wizara ya kilimo kwa maeneo yenye upungufu hasa ambao umesababishwa na hali ya hewa. “Kwa maeneo ambayo hali ya hewa ilikuwa nzuri, pale ndipo kauli ya Mheshimiwa Rais inapoingia kwamba hawakuzalisha kwa tija chakula,” alisema. Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kupeleka chakula maeneo ambayo kuna upungufu wa chakula. Rais Magufuli amewahi kutoa kauli mara kadhaa kuwa mahali ambako kutakabiliwa na njaa, basi mkuu wake wa wilaya na mkoa atapoteza wadhifa wake, hasa kwa kuwa na maeneo mengi ya kulima yana hali ya hewa nzuri na nguvukazi ipo. Akijibu swali la Mbunge Viti Maalumu, Sikudhani Chikambo (CCM), kuhusu ununuzi wa korosho msimu huu, Majaliwa alisema ununuzi huo umeanza vizuri kwa njia ya minada. Hata hivyo, alisema msimu huu hawatatumia utaratibu wa msimu uliopita ambao korosho zilinunuliwa zote na serikali kwa bei ya Sh 3,300 kwa kilo na tayari imeshatoa jumla ya Sh bilioni 40 ambazo wanaendelea kuzipokea.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Mgaya Kingoba, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi