loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

MOI yafanya upasuaji wa kihistoria kwa mwenye kifafa

KWA mara ya kwanza, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imefanya upasuaji mkubwa wa ubongo kwa mtoto mwenye kifafa.

Upasuaji huo umefanywa na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji wa mgongo, ubongo na mishipa ya fahamu wa Moi, chini ya uangalizi wa wakufunzi kutoka mataifa ya Ulaya na Marekani, wakiongozwa na bingwa wa upasuaji wa mgongo, ubongo na mishipa ya fahamu, Roger Hartl kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornel cha Marekani.

Akizungumza na HabariLEO jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Dk Respicious Boniface, alisema upasuaji huo wa ubongo kwa mtu mwenye kifafa ni mara ya kwanza kufanyika katika historia ya nchi na umemuhusisha mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

“Upasuaji huu ni mkubwa na ni wa kihistoria kwa hapa kwetu, naamini kila kitu kitaenda salama, madaktari wanafanya kwa nafasi yao, lakini Mungu pia ana nafasi yake,” alisema.

Dk Boniface alisema upasuaji huo umewezekana kutokana na kuwa na mitambo ya kisasa pamoja na kuwa na wataalamu waliobobea katika tiba hiyo kutoka nje ya nchi ambao wanawapa ujuzi kwa vitendo madaktari wa Moi.

Akizungumzia ugonjwa huo, alisema ni ugonjwa unaosababishwa na kuathirika kwa ubongo, unaojitokeza kama mchanganyiko wa kifafa na baadhi ya dalili za ugonjwa wa kudorora kwa ubongo unaopelekea waathirika kupoteza fahamu na kukakamaa viungo.

“Jambo la wazi ni kwamba si ugonjwa wa kurithi, japo huwa unatokea miongoni mwa familia, huu ni ugonjwa unaoweza kujitokeza na kupotea ,” alisema Dk Henry Humba mtaalamu wa magonjwa ya ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa Juni, mwaka huu, robo tatu ya watu walio na ugonjwa wa kifafa katika nchi zenye kipato cha chini hawapati matibabu yanayostahili, hivyo kuongeza hatari ya kufa kabla ya wakati wao.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi