loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchungaji kizimbani tuhuma ya kukutwa na meno ya tembo

JESHI la Polisi wilayani Mpwapwa limempandisha kizimbani Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Sekandi Mkombola, kwa tuhuma za kupatikana na meno ya tembo.

Akisoma hati ya mashitaka juzi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo, Nurupudesia Nassary, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Maulid Manu, alisema mtuhumiwa anakabiliwa na makosa mawili ya kupatikana na nyara za serikali na uhujumu uchumi.

Alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 4, mwaka huu katika kijiji cha Minguwi Pwaga, wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma. Manu alidai mshtakiwa alifanya kosa hilo kinyume cha sheria namba 86 ya wanyamapori ya mwaka 2009 na kifungu 57 cha sheria ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Aidha, Hakimu Mkazi Mfawidhi Nassary alisema kesi hiyo haina dhamana, hivyo mshtakiwa alipelekwa mahabusu mpaka kesi yake itakapotajwa tena Novemba 20, mwaka huu.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Mpwapwa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi