loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shein atekeleza Ilani CCM 95%

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amefanikiwa kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa asilimia 95 katika sekta muhimu za elimu, afya na mawasiliano na ustawi wa jamii.

Katibu wa Kamati maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, Catherine Peter Nao alisema hayo alipozungumza na gazeti hili ofisini kwake Kisiwandui kuhusu mafanikio ya Dk Shein katika kipindi chake cha miaka tisa ya uongozi wake.

Nao alisema ilani ya uchaguzi ya CCM ndiyo mkataba kati ya chama na wananchi waliokipigia kura hivyo lazima ione kuwa inatekelezwa ili kukidhi malengo na matarajio ya wapigakura.

Alisema baadhi ya sekta ikiwemo ya afya na elimu, Rais Shein amevuka malengo kwa wananchi kupata huduma bila ya malipo kutekeleza ahadi ya rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume. Alisema Rais Shein amefanikiwa kutekeleza na kudumisha malengo ya Karume kutoa tiba bure na elimu bure kwa vijana.

‘’Tunampongeza Rais Shein kwa kuendelea kutekeleza malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ya kutoa huduma za matibabu bure na elimu bure kwa watu wetu”, alisema Nao.

Alisema huduma za afya zimeimarishwa hadi vijijini hospitali mbili za wilaya ya Kusini Makunduchi na Kivunge Kaskazini Unguja zikipandishwa daraja na kuwa na hospitali za wilaya. Aidha alisema Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba imefanyiwa ukarabati mpya na serikali ya China na kuwafanya wananchi wa Pemba kuacha kwenda Unguja kupata huduma za rufaa.

CCM imempongeza kwa kutekeleza ahadi zake ambazo hazimo katika ilani, ikiwemo kujenga miji ya kisasa iliyopo ng’ambo.

‘’Tunashuhudia kuanza kwa mji wa kisasa na majengo yake katika mji wa Kwahani...baada ya kumalizika ujenzi huo Chumbuni kutajengwa majengo ya kisasa, hizo ni ahadi zake ambazo hazimo katika utekelezaji wa ilani,’’ alisema.

Kuhusu uteuzi, alisema amefanya kazi kubwa ya kutoa nafasi za uongozi kwa wanawake, ikiwemo kuwachagua mawaziri watano. Mawaziri watano aliowateua katika baraza la mawaziri wote amewapa wizara nyeti zenye maamuzi na uchumi wa nchi.

Mawaziri hao ni Riziki Pembe Juma, Wizara ya Elimu, Dk Sirra Ubwa Mamboya, Wizara ya Mawasiliano na Ujenzi, Balozi Amina Salum Ali anayeongoza Wizara ya Biashara na Viwanda.

Maodline Castico anayeongoza Wizara ya Wanawake na Watoto na Salama Aboud Talib wa Wizara ya Maji, Nishati na Ardhi. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa alisema Dk Shein amefanya mambo makubwa Pemba kwa kuimarisha miundombinu na ukarabati mkubwa wa Hospitali ya Abdallah Mzee.

Mberwa, ambaye ni Mwenyeviti wa wenyeviti wa CCM wa mikoa mitano ya Zanzibar, alisema jambo kubwa linalokumbukwa na wananchi wengi wa Pemba ni kuwepo kwa amani na utulivu huku wananchi wakifanya siasa bila ya vurugu wala ugomvi.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi