loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kairuki apongeza Airtel kuboresha huduma zake

KAMPUNI ya simu ya Airtel Tanzania imezindua huduma ya Airtel 4G, ikiwa ni muendelezo wa kupanua wigo wa mtandao wake nchini ili kutimiza dhamira ya kutoa huduma bora kwa wateja wake.

Akizindua huduma hiyo ya Airtel 4G jana jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughuliki Uwekezaji, Angellah Kairuki alisema kuwa ni furaha kuona Airtel inatekeleza mipango ya uwekezaji na kuja na huduma za mtandao wa Airtel 4G, kwa lengo la kukidhi mahitaji ya watanzania wote. Alisema hiyo ni ishara tosha inayoonesha mikakati ya kuijenga Airtel mpya, itakayoendelea kutoa gawio kwa wanahisaikiwemo Serikali yetu.

“Nimefarijika kusikia taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Airtel kwamba Airtel inatekeleza mikakati yao ya uwekezaji wa kuboresha huduma, kwa kuanzisha huduma hii ya 4G/LTE ikiwa na wigo mkubwa wa kutoa huduma za mawasiliano, mimi kama Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji, inanipa ishara nzuri ya matokeo ya mazingira mazuri tuliyoyaweka ili wawekezaji wetu nchini, waweze kutekeleza majukumu yao na kulipa faida taifa, haya yote yanafanikiwa chini ya uongozi wa Serikali ya Rais John Magufuli.

Alisema “Wote tunatambua Airtel Tanzania na Serikali yetu, waliingia makubaliano mazuri hivi karibuni, kwamba serikali yetu iwe na umiliki wa asilimia 49 wa hisa ndani ya Airtel Tanzania. Kutokana na makubaliano hayo, hadi leo Airtel Tanzania imeshailipa serikali jumla ya shilingi bilioni 8 kama sehemu ya makubaliano hayo. Na leo hii Airtel wanatekeleza upanuzi wa mtandao, hii ndiyo mikakati ya kuijenga Airtel mpya ili kuendelea kuleta tija kwa shughuli za kijamii na uchumi”.

Waziri Kairuki aliipongeza Airtel kwa kasi yake ya kusambaza huduma hiyo ya Airtel 4G katika miji mikubwa takribani 25, ambapo jana waliwasha mtandao wa Airtel 4G mkoani Dodoma.

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na vyombo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi