loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wabunge wa Kenya wamfagilia Magufuli

WABUNGE wa Kenya wamemfagilia Rais John Magufuli, kutokana na kusimamia vizuri mapato na matumizi na ujenzi wa miradi, ambayo thamani ya fedha inaonekana katika utekelezaji wake nchini.

Wakizungumza katika ziara nchini ya kujifunza namna Mfuko wa Jimbo unavyofanya kazi na kutembelea miradi mbalimbali jijini Dodoma, walisema Rais Magufuli ameonesha umahiri wa hali ya juu katika kazi yake, hasa ya kusimamia fedha za umma katika miraadi.

Mbunge wa Turbo na Embakasi Central, Janet Sitienei alisema wao kama wabunge wa Kenya, wanasifu utendaji wa Rais Magufuli na wanapongeza kutokana kwa kusimamia fedha za umma katika miradi na matokeo yake yanaonekana, kwani hakuna senti inayopotea.

“Asante Rais Magufuli kwa kazi na thamani ya fedha inaonekana na zinatumika katika kuendesha miradi na kila fedha inatumika vizuri,” alisema Sitienei.

Alisema miradi mikubwa kama ya reli, barabara na viwanja vya ndege, inatekelezwa kwa kusimamia fedha kutokana na usimamizi wa kiongozi huyo. Sitienei alimpongeza Raisi Magufuli, kwa umahiri wa kusimamia miradi mikubwa ya kitaifa, inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma, ikiwemo ya kuunganisha usafiri Dodoma kwa Reli, barabara, stendi, soko hadi uwanja wa ndege Msalato.

Alisema fedha zilizotolewa kwa ajili ya kujenga stendi ya mabasi zaidi ya Sh bilioni 41 na soko pamoja na ujenzi wa eneo la kupumzikia Chinangali, ni fedha nyingi, ambazo bila usimamizi mzuri wa miradi na thamani ya fedha isingeonekana.

Mbunge wa Jimbo la Embakasi Nairobi, Getrudi Mwangi alisema mwanzo alikuwa haielewi vizuri, lakini sasa baada ya kutembelea miradi mikubwa Jijini Dodoma, anaamini jiji hilo litakuwa miongoni mwa majiji bora Afrika. Mwangi alisema anaeleza hilo kutokana na mipango mingi yenye kuendeleza jiji la Dodoma ambao ni makao makuu ya nchi katika kujenga miundombinu ya barabara, reli, stendi na kuunganisha kwa barabara na reli za ndani hadi uwanja wa Ndege.

Alisema miradi hiyo inaipa sifa Dodoma kama makao makuu ya nchi, lakini pia mpango wake wa miundombinu unaionesha ni jiji lililojengwa katika Karne ya 21, hivyo kinachotakiwa ni kuhakikisha usimamizi hadi miradi inakamilika ni jambo muhimu.

Mbunge Elgon, Fred Kapondi alisema wamefurahi kusikia kwamba ramani ya Mpango Mkakati wa Mji wa Abuja, ilichukuliwa kutoka Dodoma, hivyo Abuja ni mtoto wa Dodoma na kwamba Nigeria inatakiwa kukubali kwamba imejenga jiji hilo kutokana na msaada wa jiji la Dodoma.

Kapondi alisema miradi mikubwa inayotekelezwa Dodoma, inaonesha kwamba serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba jiji hilo linalojengwa katika Karne ya 21, linakuwa bora zaidi barani Afrika. Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe alisifu ujio wa Wabunge hao kutoka Kenya na kutembelea ofisini kwake.

Alisema wamepokea ushauri kutoka kwa wabunge hao, kwamba ili miradi hiyo iwe endelevu wanatakiwa kuwa na mfumo bora wa usimamizi bora wa miradi hiyo mikubwa kitaifa na makao makuu ya nchi.

Awali, Mkurgenzi wa Jiji Godwin Kunambi alisema Jiji la Dodoma lilipokea kutoka serikali Sh bilioni 77 na sasa baadaye serikali iliongeza Sh bilioni tisa ambazo zinatumika katika kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwemo soko, stendi na uwanja wa Msalato na itaunganishwa kwa barabara na reli.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi