loader
Dstv Habarileo  Mobile
TRA yahimiza ulipaji kodi ya majengo

TRA yahimiza ulipaji kodi ya majengo

MWITO umetolewa kwa wananchi kulipa kodi ya majengo kwa kuwa viwango vilivyopangwa katika kodi hiyo ni rafi ki na vinalipika kwa urahisi ikilinganishwa na hapo awali.

Mwito huo ulitolewa na Ofisa Kodi Mkuu, Julius Mjenga, kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakati wa kampeni ya usajili, huduma na elimu kwa mlipakodi katika kata ya Mlimba, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.

Mjenga alisema kwa sasa viwango vya kulipia kodi ya majengo ni Sh 10,000 kwa nyumba ya kawaida, Sh 50,000 kwa kila sakafu ya ghorofa katika majiji, miji na manispaa na Sh 20,000 kwa ghorofa zima katika halmashauri za wilaya.

“Katika majiji, manispaa na halmashauri za miji, iwapo kuna nyumba zaidi ya moja kwenye kiwanja kimoja, kila nyumba itatozwa Sh 10,000 wakati katika halmashauri za wilaya, endapo kiwanja kimoja kina nyumba zaidi ya moja, nyumba yenye thamani ya juu ndio itakayohesabika na kutozwa Sh 10,000,” alisema.

Aidha, Mjenga alisema majengo yasiyotozwa kodi ya majengo ni pamoja na nyumba zilizoezekwa kwa nyasi na makuti, nyumba zilizojengwa kwa udongo na majengo ya ibada kama vile misikiti na makanisa.

  1. Aidha, alisema wazee wenye miaka 60 na kuendelea wamesamehewa kulipa kodi ya majengo kwa nyumba moja ambayo wanaishi na wazee hao wanapaswa kufika ofisi za TRA kuomba kusamehewa kodi hiyo. TRA inaendelea na kampeni ya usajili, huduma na elimu kwa mlipakodi katika mikoa ya Morogoro na Pwani na itamalizika Novemba 17, mwaka huu.
https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/75e961546e9cdef6587449494d3f0793.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi