loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Taifa Stars kazi moja leo

MALENGO ya timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars ni kupata ushindi katika mechi ya leo dhidi ya Equatorial Guinea na kujiweka vizuri katika mechi dhidi ya Libya siku nne zijazo.

Stars leo itakuwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam saa moja uisku kuikaribisha Equatoria Guinea katika mechi ya kwanza ya kundi J kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika, Afcon 2021 Cameroon.

Mchezo huo unaumuhimu kwa stars kupata ushindi utakatengeneza mazingira ya kufanya vyema kwenye michezo inayokuja ya kundi hilo ambapo pia kuna timu ya Tunisia. Katika viwango vya ubora vya Fifa mwezi uliopita, Tanzania na Equatorial Guienea ndizo zinazoonekana kuwa kwenye nafazi za chini, Tanzania ikiwa ya 133 na Equatorial Guinea ni wa 135, Libya ni ya 103 na Tunisia ya 29.

Pamoja na kwamba Stars wako nyumbani kiasi cha kupewa asilimia kubwa ya kutumia faida hiyo katika mchezo huo lakini bado wapinzani wao wanakikosi bora ambacho kimesheheni wachezaji wengi wanaocheza soka nje ya nchi ikilinganishwa na Tanzania yenye wachezaji sita wanacheza soka ughaibuni waliojumuishwa kwenye kikosi hicho.

Kocha wa Stars Etienne Ndayiragije alisema maandalizi yamekamilika vyakutosha na malengo yao ni kupata matokeo yatakayowapa mwanga kujipanga na mchezo wao unaofuata wa kundi hilo dhidi ya Libya.

Alisema anaimani kubwa kuwa wachezaji wake hawawezi kumuangusha kulingana na mazoezi na mbinu walizopewa.

“Maandalizi kama wenyeji yamekamilika vyakutosha na malengo yetu ni kupata ushindi utakaotupa mwanga na nguvu ya kujipanga na mchezo unaokuja wa kundi dhidi ya Libya utakaochezwa siku nne baada ya mechi ya kesho (leo) ugenini” alisema Ndayiragije.

Alisema wachezaji wote wanaounda kikosi hicho afya zao zipo sawa hivyo wamesaliwa na kazi ya kutafuta matokeo kuendelea kuwapa furaha watanzania lakini pia kujitengenezea mazingira katika kundi.

Aidha Stars wanaingi kwenye mchezo huo na ari ya ushindi baada ya kutoka kushinda mchezo uliopita dhidi ya Sudan na kukata tiketi ya kushiriki fainali za Mabingwa Afrika, Chan ambayo hushirikisha wachezaji wa ndani itakayofanyika Cameroon mwakani. Huku wapinzani wao Equatorial Guinea wanaingia kwenye mchezo huo wakitoka kupoteza kwa jumla ya mabao 3-2 dhidi ya timu ya Congo Brazzavile mchezo uliokatisha ndoto zao za kushiriki Chan.

Kikosi cha stars kinaingia kwenye mchezo huo huku matumaini makubwa yakielekezwa kwa nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta anayecheza Ubelgiji na Simon Msuva anayecheza Morocco kulingana na mchango wao wanaoutoa kwenye timu hiyo hususani kwenye kuamua matokeo.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi