loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kili Queens yapania kuweka historia

KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara Kilimanjaro Queens, Bakari Shime amesema wanataka kuweka historia mpya katika michuano ya chalenji ya Afrika Mashariki na Kati kwa kuchukua kombe kwa mara ya tatu mfululizo.

Michuano hiyo itakayoshirikisha nchi nane za Afrika Mashariki na Kati inatarajiwa kutimua vumbi kuanzia kesho kwenye viwanja vya Azam Complex Chamazi. Timu zitakazoshiriki ni Tanzania, Burundi, Djibouti, Zanzibar, Sudan Kusini ,Kenya, Uganda na Ethiopia.

Michuano hiyo inasimamiwa na Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na hii ni mara ya tatu inafanyika. Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Shime alisema wamejipanga kubakisha kombe hilo walilolitwaa mara ya mwisho mjini Kigali, Rwanda na hivyokuhimiza watanzania kujitokeza kwa wingi ili kuwa sehemu ya historia hiyo.

“Tunajua sio rahisi ila tumejipanga katika ugumu huo kuchukua kombe hilo mfululizo, kila mtanzania ajitokeze uwanjani awe sehemu ya historia tunayokwenda kuiweka katika michuano hiyo,” alisema.

Alisema maandalizi yao yamemalizika na kwamba wako katika matayarisho ya mwisho kuweka miili ya wachezaji vizuri kujiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan Kusini utakaochezwa kesho Chamazi. Mmoja wa wachezaji wa kikosi hicho Fatma Isa ‘Fetty densa’alisema kutokana na maandalizi waliyofanya muda mrefu ana imani watafanya vizuri kwasababu wako katika morali ya hali ya juu.

“Tumejiandaa vizuri, tuko katika morali ya kutosha watanzania wategemee matokeo mazuri kutoka kwetu, yeyote atakayetokea mbele yetu tuko tayari kwa mapambano, muhimu watanzania waje kutuunga mkono kama wanavyofanya kwa wanaume kwa kuwa tunaweza,” alisema.

Tanzania imepangwa kundi moja na Zanzibar, Sudan Kusini, Burundi na Djibouti. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya ndani ya michuano hiyo, Athumani Nyamlani maandalizi yote yamekamilika na timu zote shiriki zimeshawasili.

“Mpaka leo (jana) saa 12 jioni ndio timu ya mwisho Zanzibar imewasili, kwa hiyo maandalizi yapo vizuri na tunatarajia kuwa na mashindano mazuri na yenye msisimko,” alisema Nyamlani ambaye ni makamu wa rais wa Shirikisho la soka Tanzania, TFF.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi