loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kili Queens kanyaga twende

UIMARA wa safu ya ulinzi kwa timu ya soka ya Tanzania Bara ya Wanawake, Kilimanjaro Queens, umakini wa kutumia nafasi kwa mipira iliyokufa na safu bora ya ushambuliaji ni moja ya mambo yayoweza kuwafanya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Sudan Kusini utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Dar es Salaam.

Queens inayonolewa na kocha mzalendo Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ kwa siku za hivi karibuni imekuwa na kiwango bora baada ya kufanya vizuri kwenye michezo iliyopita, ikiwemo kubeba taji la michuano ya Cosafa iliyofanyika mwaka huu nchini Afrika kusini.

Hata hivyo ubora wa kikosi hicho umekuwa ukionekana kwenye safu ya ushambuliaji, hivyo wana changamoto kubwa ya kuhakikisha wanaendeleza hilo, kwani katika michezo iliyopita ya kimashindano , wachezaji wa timu hiyo walikuwa wakifunga katika kila mchezo.

Kikosi hicho kilipokuwa Afrika Kusini kilicheza michezo walicheza michezo sita, ambapo walifanikiwa kufunga mabao 13 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara tatu waliibuka na ushindi wa mabao 2-1, Zambia 13 Afrika Kusini 0-2 Tanzania, Zambia 2-1 Tanzania, Tanzania 8- 0 Eswatin na kisha Botswana 0-2 Tanzania.

Kwa takwimu hizo, Queens ambao ni mabingwa watetezi wa (Cecafa) wana kila sababu ya kuendeleza rekodi hizo kwakuwa ukanda wa Cosafa upo juu kwenye soka la ushindani la wanawake ikilinganishwa na ule ea Afrika Mashariki na Kati.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha Bakari Shime alisema maandalizi ya kikosi hicho yamekamilika kwa asilimia 95 kuingia kwenye michuano hiyo wakianza kwa kuwakabili Sudan leo ilikupata ushindi utakaowafanya kuendeleza kampeni zao za kutetea taji hilo.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika kwa asilimia 95 kwa kikosi changu kwa kuwakabili wapinzani wetu ,hivyo hatuna cha kupoteza zaidi ya kutafuta ushindi utakao tufanya kujiweka sawa kwenye kundi” alisema Shime.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi