loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru yachunguza upotevu wa mamilioni ubalozi Tanzania nchini Ethiopia

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru), imeanza uchunguzi kuhusu upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuikabidhi taasisi hiyo jalada la uchunguzi wa upotevu wa fedha hizo, ambazo hadi jana bado ilikuwa haijajulikana ni kiasi gani.

Jalada hilo limekabidhiwa Takukuru na Katibu Mkuu wa Wiz- ara ya Mambo ya Nje na Ush- irikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe ambapo alimkabidhi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika ofisi ndogo za Wizara hiyo ya Mambo ya Nje, Dar es Salaam huku Mkurugenzi huyo wa Takukuru akibainisha kuwa kiasi cha fedha kilichopotea, kitawekwa hadharani baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

Alisema,“hii ni hatua nzuri na kubwa katika vita dhidi ya mapambano ya rushwa hapa nchini, kwa kuwa kwa sasa tunaona wizara inatuwasilishia nyaraka muhimu zitakazotuwezesha kubainisha mengi kuhusiana na mazingira ya rushwa katika ubalozi huo.”

Uchunguzi huo unafanyika baada ya kubainika kuwepo kwa matumizi ya fedha yasiyoeleweka, ambapo haijajulikana bado kama fedha hizo zilipotea au ni matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Kwa upande wake, Dk Mnyeti alibainisha kuwa hatua hiyo imekuja baada ya Rais John Magufuli kuweka msisitizo kuhusu matumizi bora ya fedha iwe kwa taasisi za nchini na nje ya nchi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi