loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kalemani: Tanesco hakikisheni mnazalisha megawati 10,000

WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani ameiagiza bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini humo (Tanesco), kuhakikisha Tanzania inaangaziwa na nishati ya umeme, kwa kuhakikisha ifi kapo mwaka 2025 megawati 10,000 zinazalishwa.

Pia amewataka kusimamia ukusanyaji wa mapato hadi kufikia Sh bilioni 60 ili shirika hilo liweze kujiendesha kwa ufanisi. Aidha, ameiagiza Bodi hiyo kwenda kukata umeme kwa wadaiwa wote sugu bila kujali mtu wala wadhifa wake.

Dk Kalemani alitoa agizo hilo jana Jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Bodi ya Tanesco iliyotekuliwa Novemba 13, mwaka huu. Alisema ili kufikia hilo, ni lazima bodi ikasimamie miradi yote ya umeme iliyoanza kutekelezwa na ambayo inatarajia kutekelezwa.

“Hakikisheni miradi yote inayotekelezwa inakamilika kwa wakati uliopangwa, ikiwamo mradi wa Mwalimu Julius Nyerere ambao utatupatia zaidi ya megawati 2,000 na mkandarasi anatakiwa kuukabidhi Juni 2022, hatutaongeza muda, saa wala dakika katika mradi huu” alisema.

Dk Kalemani pia aliitaka bodi hiyo, kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa miradi yote ya njia ya kusafirishia umeme ili maeneo yote ya nchi yaunganishwe na gridi ya taifa.

‘Pamoja na majukumu yenu kwa mujibu wa sheria, na- taka nipate taarifa ya utekelezaji wa majukumu yenu kila baada ya miezi mitatu,”alisema Dk Kalemani.

Dk Kalemani pia aliitaka bodi hiyo, kushughulikia kero katika maeneo mbalimbali, ikiwamo suala la baadhi ya maeneo kukosa umeme kwasababu ya kurekebisha umeme. na kusisitiza ni lazima watanzania wapate umeme kwa saa 24. Pia aliiagiza bodi hiyo kusimamia Wakala wa Kupeleka Umeme Vijijini (REA) na wakandarasi, kuhakikisha umeme unafikishwa vijijini ili kutimiza malengo ya serikali Aidha, Dk Kalemani pamoja na kuipongeza Tanesco kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Sh bilioni 9 hadi bilioni 46 kwa wiki, alitaka eneo hilo litiliwe mkazo.

“Mkaongeze makusanyaji wa mapato zaidi, sasa mmeweza kukusanye shilingi bilioni 47 kwa wiki, mkifikisha umeme kila eneo na kuja na ubunifu wa vyanzo vingine mnaweza kufikisha makusanyo ya shilingi bilioni 60 kwa wiki”alisema Dk Kalemani.

Katika hatua nyingine, Dk Kamelani ameagiza bodi hiyo, kuhakikisha inawakatia umeme wadaiwa sugu wote bila kujali, kama ni taasisi za serikali au za watu binafsi. “Nendeni mkahakiki madeni yote ya wateja na kama kuna wadaiwa sugu wakatieni huduma bila huruma, ni lazima shirika lipate fedha za kujiendesha haiwezekani watu wanadaiwa fedha nyingi na hawataki kulipa kwa wakati,” alisema Dk Kalemani.

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi