loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watoto waibuka na muziki wa Babu Magufuli

SANAA ya muziki hupendwa na watu wa rika zote kwa maana ya watoto, vijana na wazee. Wapo wanaozaliwa na vipaji vyao vya kuimba, wapo wanaorithi kizazi hadi kizazi labda mama, baba, babu au bibi katika familia waliwahi kuwa wanamuziki lakini pia, wapo wanaojifunza. Lakini yote kwa yote, muziki ni burudani ndio maana wanaousikia ukipigwa wapo watakaotikisa kichwa kulingana na ujumbe utakavyomkuna, wapo watakaoinuka kucheza na wengine watacheza wakiwa wamekaa. Mbali na burudani hufundisha, kuelimisha na kukosoa inategemea na ujumbe wake.

WASANII WATOTO

Hivi sasa kuna watoto wawili wa Abdallah Issa wameamua kujiingiza katika muziki wa kufoka maarufu kama ‘hip hop’ lakini ndani yake wakijitahidi zaidi kuimba maendeleo yaliyofanywa na kiongoza wa nchi Rais John Magufuli. Wameamua kuja na kitu tofauti kulingana na walivyoguswa na kile, ambacho Rais Magufuli amekuwa akikifanya kila siku katika kuleta maendeleo.

Watoto hao ni Mnora Abdallah ambaye ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 11 anayesoma darasa la tano shule ya msingi Vingunguti na Nasra Abdallah mwenye umri wa miaka 15 anayesoma kidato cha pili shule ya sekondari Kinyamwezi Chanika. Wameachia wimbo wao unaitwa Babu Magufuli kusifia maendeleo yaliyofanywa na kiongozi huyo wa nchi katika kipindi alichokaa madarakani wakisema wamevutiwa na utendaji kazi wake.

ASEMAVYO NASRA

Nasra aliyeambatana na mdogo wake Mnora pamoja na baba yake kwenye ofisi za magazeti ya serikali zinazocapisha HabariLeo, Daily News na SpotiLeo zilizopo Tazara Dar es Salaam anasema anapenda jinsi Magufuli anavyobadilisha nchi kwa maendeleo kwa kila sekta.

“Napenda kuona anavyoleta maendeleo, amejenga madaraja, barabara hata kwenye shule tunaona baadhi ya vitu viko tofauti, kwa kweli anafanya juhudi kubwa kukuza uchumi wa nchi,” anasema.

Anasema kuimba kwao muziki wa kumsifu kiongozi huyo ni kumtia moyo ili aendeleze jitihada zake lakini ajue kuwa hata wao kama watoto wanathamini kile anachokifanya. Msichana huyo anasema huo ni wimbo wao wa kwanza wamefanya na mdogo wake wakiwa wanasimamiwa na baba yao ambaye pia, ni msanii wa sanaa za asili na mwigizaji japo si maarufu.

ATAMANI MAKUBWA

Anasema anatamani kufanya makubwa katika sanaa yake wakati akiendelea na masomo kwani vyote vina umuhimu mkubwa katika maisha yake lakini anabainisha kuwa bado hukabiliwa na changamoto hasa kifedha. Miongoni mwa wasanii wakubwa wanaomvutia na kutamani kufikia mafanikio yake ni Faustina Charles ‘Nandy’ akisema ana sauti nzuri na hata nyimbo zake ni nzuri pia.

MNORA ANASEMA

Kwake Mnora ukimtizama machoni anaonekana mjanja ila mwenye aibu, lakini mambo aliyoyafanya katika muziki wake ni makubwa. Kuimba sio kazi rahisi lakini ameonesha uwezo wake wa kuimba sambamba na dada yake pasipo kuogopa huku akimshukuru baba yake kwa kujaribu kuwa pamoja nao na kuwaunga mkono katika juhudi zao za kuendeleza sanaa hiyo. Anasema wimbo huo wametungiwa mashairi na baba yao, ambaye amekuwa akipenda pia muziki na akitamani watoto wake wafike mbali hapo baadaye baada ya kumaliza masomo yao.

“Ukweli baba yetu amekuwa pamoja nasi kutuunga mkono nasi tunatamani kufika mbali ndio kwanza tunaanza safari ya muziki na wimbo wetu wa Babu Magufuli ndio kwanza, tunatarajia kufanya mengi baadaye kulingana na mapokeo yetu katika jamii,” anasema.

Anasema yeye kama mtoto anaona mambo mengi mazuri yanayofanywa na Rais Magufuli hivyo, kuimba muziki wenye ujumbe wa kumsifu ni fahari kwake. Mtoto huyo anasema anasiku hizi hawapigwi sana. Ndipo na yeye akamwambia ni Rais wa awamu ya tano kwa hiyo akaona ni watoto wanaojaribu kufuatilia mambo.

CHANGAMOTO

Anasema kwa wasanii wanaoanza hupata wakati mgumu wa kukubalika haraka akihimiza jamii kuwapokea vijana wake ili waweze kutimiza ndoto zao. Nyingine anasema mitaji ya kuingia studio na kupata nafasi ya kutambulika ni ngumu pia.

MALENGO YAO

Anasema wameanza hivyo taratibu wanategemea kama watapokelewa vizuri basi baadaye waanzishe bendi ila katika kufanikisha hilo wanaomba ufadhili kutoka kwa wadau mbalimbali.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi