loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SMZ kuendelea kuenzi, kutunza wazee

Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, amesema kuwa Serikali anayoiongoza, itaendelea kuwatunza na kuwaenzi wazee ikiwemo kuimarisha huduma za kiuchumi na kijamii ili waishi kwa furaha.

Amesema hayo jana kwa nyakati tofauti katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, alipozungumza na wazee wa wilaya za kichama za Amani na Mjini.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeandaa Sera ya Wazee na hivi sasa inaandaa sheria ya kuwatunza wazee na kuwaenzi wazee.

Hivyo, alisema utaratibu wa kuwatunza wazee, kwa kuwekwa taratibu na kanuni, utafanyika na kwa wale wasiokuwa na vitambulisho vikiwemo vyeti vya kuzaliwa watajumuishwa.

Alieleza kuwa serikali yake inasimamia na kuendesha programu maalum ya Pencheni Jamii.

Kwamba program hiyo ya pensheni, imeagizwa na CCM katika Ilani yake ya Uchaguzi na alichokifanya yeye ni kutekeleza agizo hilo.

Alisema kuwa uwezo ukiruhusu, ataongeza pensheni hiyo kabla ya kuondoka madarakani.

Shein alieleza haja ya wazee, kuwaeleza vijana kuheshimu wazee na vipi wazee wanatakiwa kuenziwa na kutunzwa na kuwapa heshima yao, kutokana na mambo makubwa waliyoyafanya.

Rais Shein alisema kuwa serikali ya Zanzibar inathamini na inajali juhudi za wazee, walizozichukua hadi kupatikana uhuru wa Tanganyika na uhuru wa Zanzibar kupitia vyama vya ASP na TANU.

Alisema kuwa wazee ndio walioijenga Zanzibar na kuleta ukombozi na kuwakomboa wanyonge.

Kwamba ipo haja ya kupokea mawazo ya wazee, kuwaheshimu na kuwalinda wazee, kwani kuna kila sababu ya kufanya hivyo, hasa ikizingatiwa historia ya wazee wa nchi hii.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi