loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania, Angola zajadili ushirikiano mafuta, gesi

WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amekutana na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro De Oliveira na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika utafi ti wa mafuta na gesi na ununuzi wa mafuta.

Mazungumzo kuhusu ushirikiano huo, yalifanyika juzi mjini hapa na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa petroli na gesi, Marwa Petro, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk James Mataragio na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Angola nchini.

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Angola, kwa kuwa tayari ina uzoefu kwenye masuala ya utafiti wa mafuta na gesi na tayari imeshagundua mafuta.

Aliongeza kuwa Tanzania ina maeneo kadhaa yenye viashiria vya mafuta, mfano Bonde la Eyasi Wembere na Ziwa Tanganyika, hivyo serikali inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kuwa nchi inapata mafuta kama ilivyo kwa Angola, ambayo ipo pia katika Umoja wa Nchi zinazozalisha Mafuta Duniani (OPEC).

Alitoa muongozo wa nini kinachotakiwa kufanywa, baada ya mazungumzo ya viongozi hao wawili ili lengo hilo la ushirikiano liweze kufanyiwa kazi na wataalamu wa nchi hizo mbili, likiwemo suala la Angola kuiuzia mafuta Tanzania.

Balozi Oliveira alisema wakuu wa nchi za Angola na Tanzania, wanafahamu kuhusu suala hilo, hivyo ni muhimu kwa watendaji wa pande zote mbili kulifanyia kazi suala hilo na kutoa taarifa kwa viongozi hao wakuu, badala ya kusubiri viongozi hao kuulizia utekelezaji wa suala hilo.

Wakati huohuo, Waziri wa Nishati, Dk Kalemani alikutana na watendaji wa kampuni ya ORMAT ya Marekani ambao wameeleza nia ya kampuni hiyo kushirikiana na Taasisi ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika masuala ya utafiti na uzalishaji umeme kwa kutumia jotoardhi.

Meneja Mwandamizi wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Raphael Swerdlow alimueleza Kalemani kuwa kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1965, inazalisha umeme kutokana na jotoardhi kwenye maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Kenya, ambapo wanazalisha megawati 139.

Waziri Kalemani aliwaeleza watendaji wa kampuni hiyo kuwa serikali inahitaji kampuni makini na yenye nia ya dhati ya kushirikiana na TGDC, kuweza kuzalisha umeme kutokana na chanzo hicho, ambacho hakijaanza kuzalisha umeme nchini, licha ya kuwa na maeneo mengi nchini yenye viashiria vya jotoardhi.

SHIRIKA  la Madini Nchini (Stamico) litaanza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu,Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi