loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkapa- Sikuchukia wana- CCM matajiri

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amesema hakuwachukia wanasiasa matajiri waliokuwa ndani ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) lakini pia hakukumbatia walioingia kwenye chama hicho kwa lengo la kujinufaisha.

Mkapa amebainisha hayo katika kitabu chake kinachohusiana na maisha yake wakati akiwa mtumishi wa umma, kiongozi wa serikali, mwanasiasa na hadi kufikia ngazi ya urais kiitwacho“My Life My Purpose”

Katika kitabu hicho Mkapa anaeleza kuwa hakupenda kuona watu wakichaguliwa kugombea nafasi za kisiasa hasa ubunge kutokana na uwezo wao wa kifedha, lakini alifafanua kuwa hamaanishi wenye fedha wasipatiwe nafasi za uongozi kwenye medani za siasa.

Katika ukurasa wa 132 sura ya 11 ya kitabu hicho, Mkapa amebainisha jinsi alivyowaondoa matajiri kwenye kuwania nafasi za ubunge ndani ya CCM ikiwa ni kufuata mwenendo wa Mwalimu Julius Nyerere katika kuwaweka mbali matajiri kupata nafasi za uongozi. Hiyo ni katika kuepusha rushwa kwenye uongozi.

Anabainisha jinsi alivyolazimika kuliondoa jina la Mfanyabiashara Yusuph Manji katika orodha ya majina ya waliopendekezwa kuchaguliwa kuwania ubunge katika jimbo la Kigamboni.

Alisema pia lilikuwapo jina la mwanasiasa Abdulaziz Mohamed Abood.

Kuhusiana na jina la Manji alibainisha kuwa aliliondoa kwa kuwa hakuwahi kumuona kwenye shughuli zozote za siasa za CCM huku pia hakuwa mwanasiasa aliyejishughulisha kikamilifu katika shughuli za chama.

Mkapa alikwenda mbali zaidi na kuandika kuwa anakerwa na tabia za rushwa zinazoombwa na watendaji wa ngazi mbalimbali ili wawasaidie wananchi maskini kupata huduma kama vile huduma za afya na elimu.

Alisisitiza kuwa hakuna rushwa inayomkera kama rushwa ya maskini kutoa fedha ili apatiwe huduma za afya.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimekubaliwa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi