loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mali za wabunge, majaji zahakikiwa

Mali za wabunge, majaji zahakikiwa

SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imehakiki mali za wabunge zaidi ya 132 na majaji 46 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Harold Nsekela aliponzungumza na HabariLEO kuhusiana na utaratibu wa kuhakiki mali za viongozi uliofanyika kwa kipindi cha wiki mbili.

“Tulipanga tukutane na wabunge 181, mpaka jana (Alhamisi) tulipata nafasi ya kukutana na wabunge 132, ingawa sina takwimu ya mpaka leo (Ijumaa) maana utaratibu wa kuwahoji wabunge unaendelea.

“ Kwa upande wa majaji, utaratibu wa kuzungumza nao umekwenda vizuri katika maeneo yote ambayo maofisa waliweza kukutana nao,” alisema.

Akifafanua zaidi, Jaji Nsekela alisema katika uhakiki wa mali walioufanya kwa wabunge na majaji hao pamoja na mambo mengine wametilia mkazo kuangalia suala la mgongano wa maslahi kwa viongozi hao.

“Na eneo kubwa ambalo tunalishughulikia sasa hivi kwa viongozi wote ni suala la mgongano wa maslahi, sisi kama sektratieti tulianza kulifanyika kazi tangu mwaka jana, ni jambo ambalo kwa takribani mwaka mmoja na nusu tulishughulikia sana kwa namna ya kulizuia na kutoa elimu.”

Jaji Nsekela alisema pia wamefanya mazungumzo na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambao majaji waliohakikiwa mali zao ni wale walioko kwenye mikoa ambayo Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Mahakama Kuu ya Tanzania zina ofisi.

Alitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Mbeya, Tabora, Mwanza, Arusha Dodoma na Mtwara.

“Huko nyuma tulikuwa tunawafuata katika makazi yao na kufanya mahojiano nayo, njia hii ilikuwa na gharama kubwa, kwa njia tunayotumia sasa tumewapata wabunge hapa hapa na tumehojiana kuhusiana na tamko, na jambo la msingi tunalolifuatilia ni la mgongano la maslahi.”

Alisema mwaka jana Serikali ilitoa Sh milioni 500 kwa ajili ya kufanya uhakiki kwa nchi nzima, na takribani viongozi wa umma 400 walihakikiwa mali zao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/477e32d898b9b3c7a939714cf2591e36.jpg

POLISI Mkoani Mtwara imikamata watu 15 kwa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi