loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkapa ataja mali zake

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa ameeleza alivyopata mali na kugusia anavyozitumia kuendesha maisha yake.

Mkapa ameweka wazi kuhusiana na mali hizo kwenye kitabu cha “My Life My Purpose” hasa katika sura ya 15, ukurasa wa 220.

Ameweka bayana kuwa ana nyumba aliyoinunua akiwa madarakani iliyopo See View, Upanga, Dar es Salaam nyingine ipo Lupaso kijiji alichokulia, Mtwara ana makazi Lushoto mkoani Tanga, shamba la miwa Morogoro na mkewe Anna Mkapa amenunua ardhi Kigamboni na eneo la kufugia lililopo Bunju Dar es Salaam.

Kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza, katika sura hiyo ya 15 ambapo pia Mkapa amezungumzia namna alivyostaafu nafasi yake ya uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Jakaya Kikwete na kueleza mali alizoanzia nazo maisha na alivyoanza maisha mapya baada ya kustaafu urais.

Akianza kuzungumzia kuhusiana na mali hizo namna zinavyomsaidia amesema alijua nyumba yake ya Upanga ingemsaidia kuongeza kipato kwa njia ya kuikodisha.

Kuhusiana na nyumba ya Lushoto alisema kuwa aliwahi kumtembelea mmoja kati ya mawaziri wake aliyekuwa akiishi Lushoto aliyemwelezea kuwa nyumba iliyopo kwenye eneo hilo ilikuwa ikimilikiwa na mmoja kati ya wapigania uhuru wa zamani ambaye baada ya kufariki dunia watoto wake hawakuafikiana ni nani amiliki mali.

Alisema kuwa watoto hao walikuwa ni kama wamelitekeleza eneo hilo huku nyumba ikianza kuchakaa lakini kwa siku kadhaa walikuja kuamua kuliuza.

Alisema kuwa hapo ndipo alipoamua kulinunua eneo hilo na kutumia akiba zake za fedha na kisha kuikarabati nyumba hiyo ambayo huwa anakwenda kupumzika.

Alisema kuwa huwa anaitumia nyumba hiyo kama mahala pake na kupumzikia, kutafakari mambo mbalimbali na kuandika kwa kutumia ‘laptop’ yake na vidole vitatu kuandika huku akitania kuwa hajui kama bado anakumbuka kuandika mashairi siku hizi.

Alisema katika nyumba hiyo ana maktaba kubwa iliyosheheni vitabu kadhaa kwa kuwa anapenda kusoma vitabu hasa kusoma kuhusiana na wasifu wa watu.

Pia alisema kati ya vitabu alivyovipenda ni kitabu kilichoandikwa na aliyewahi kufanya kazi wakati wa ukoloni hapa nchini ambacho kinaelezea maisha yalivyokuwa wakati huo.

Pia alisema kuwa kwa kujifurahisha hupendelea kusoma vitabu vya habari za uchunguzi kutokea kwenye vitabu vilivyoandikwa na waandishi kama akina Henning Mankell, Agatha Christie na Edmun Bentley. Pia anapenda kumsoma PG Wodehouse.

Alisema kuwa kusoma vitabu kunampatia faraja zaidi kitu ambacho anakipenda, lakini alibainisha kuwa yeye sio mpenzi wa kuangalia filamu hasa zile zinazohusiana na mapigano.

Kuhusiana na shamba la Morogoro alibainisha kuwa lilikuwa linamilikiwa na aliyekuwa Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shule ya Shaaban Robert, shule ambayo yeye Mkapa kabla hajawa rais alikuwa mjumbe wa Bodi ya shule hiyo.

Alisema baada ya muda Katibu huyo aliyekuwa ana asili ya kihindi aliamua kuondoka nchini na kuwaachia shamba watoto wake ambao nao pia walipoamua kuondoka walimuuzia shamba hilo Mkapa.

Shamba hilo ni kati ya mashamba ya miwa yanayozalisha na kuuza miwa ambapo Mkapa alibainisha kuwa halimuingizii fedha nyingi ila anapenda kulitembelea kila mara.

Mbali na mali hizo, pia Mkapa alielezea namna alivyojihusisha na masuala ya utalii ambapo alisema kuwa alifuatwa na Dk Patrick Bergin kutokea Taasisi ya Wanyamapori Afrika alimyetaka ajiunge na bodi yake ambayo tayari kulikuwa na mtu kama vile Sir Quett Ketumile Masire aliyekuwa mjumbe.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

1 Comments

  • avatar
    Ibrahim mbuzini
    18/11/2019

    Ni jambo jema,kwa kiongozi kwa ngazi yake kwa kutoa kitabu chenye mengi ya kujifunza,Maisha Ni shule na hivyo tunajifunza kila siku.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi