loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Sijawahi kuona uwekezaji kama shambani kwa Pinda'

WANACHAMA wa Chakula Salama (Slow Food) Mkoa wa Arusha, wamesema uwekezaji uliofanywa kwenye shamba la Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ni kielelezo tosha kuwa Watanzania wana uwezo wa kutoka pale walipo kwa kutumia raslimali zinazowazunguka.

Wamesema hayo wakati wa kikao cha pamoja baada ya ziara ya mafunzo katika shamba la Waziri Mkuu Mstaafu Pinda lililopo eneo la Zinje (Zuzu) nje kidogo ya Jiji la Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya ya kundi hilo, Kiongozi wa msafara huo, Rose Machange alisema hajawahi kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa katika eneo moja kama huo.

“Hatujawahi kuona sehemu nyingine yenye vitu vingi vya pamoja ni uwekezaji wa mfano, Watanzania lazima tujifunze kupitia hili,” alisema. Kundi hilo lilijionea ufugaji wa kuku wa asili, ufugaji nyuki, kilimo cha mboga na matunda.

Alisema kiongozi huyo alisema kwa kuona shamba la Pinda wamebaini kuwa Tanzania ina raslimali nyingi ambazo zikitumika ipasavyo zitaweza kuondolea wananchi umaskini.

Mratibu wa Slow Food mkoa wa Dodoma, Amandus Chitopela alisema ziara hizo za kimafunzo zimelenga kujifunza masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha ulimaji wa vyakula na matunda ya asili.

Alisema pamoja na wanachama wa Arusha kufanya ziara hiyo nao wa Dodoma watapata nafasi za kutembelea mikoa mingine ili kuhakikisha kwamba Kilimo cha vyakula vingi vya asili kinaendele akuhsamiri kwa manufaa ya wananchi na jamii.

“Tunafikiria kuwa na maonesho ya vyakula vya asili kwa siku za usoni,” alisema. Hata hivyo, Chitopelo alisema mwamko kwa wajasiriamali wa Dodoma kujiunga katika chama hicho bado ni mdogo licha ya kuwa kiingilio ni kidogo cha Sh 25,000 .

“Kwa Dodoma kuna kikundi kimoja chenye wanachama 20 lengo ni kuhakikisha vyakula vya asili kama uwele, karanga, mlenda, mboga nyingine za majani za aina mbalimbali na matunda ya asili vinaendelea kuwepo” alisema.

Chitopela alisema kikundi Cha Dodoma kinachojulikana Ndigwa Convivium, kila mwaka kimekuwa kikiandaa mpango kazi kulingana na malengo ya Slow Food International.

Aidha wanasaidia shule ambazo zina bustani kwa kuwapa elimu kwenye filosofia ya slow food ambapo miongoni mwa shule hizo ni Marie de Matius ambayo ina bustani ya mboga na matunda.

Alisema wanachama wamekuwa wakitembelea nchi mbalimbali kujifunza na kuona jinsi gani nchi nyingine zinaendesha kilimo cha mbogamboga na matunda ya asili.

Alisema kihistoria, vuguvugu la vyakula vya asili , Slow Food duniani,lilianzishwa na Carlos Petrini wa Italia mwaka 1989 ili kukabiliana na vyakula vya haraka (fast food) ambavyo vimeonekana kuwa na madhara kwa jamii.

SERIKALI imesema nchi ina chakula cha kutosha, lakini kuna uwezekano ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi