loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bunge laombwa kusaidia wajane kurithi ardhi

Bunge laombwa kusaidia wajane kurithi ardhi

BUNGE la Tanzania limeombwa kuunga mkono kampeni ya kuondoa mfumo dume unaowanyima haki ya kurithi ardhi wanawake wanapofi wa na waume zao.

Ombi hilo limetolewa na asasi 12 zinazojishughulisha na kutetea haki za wajane kurithi ardhi kwenye mafunzo yaliyowakutanisha na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Akitoa ombi hilo Ofisa Programu wa Asasi ya Tanzania Land Alliance (TALA), Jamal Kafumbee aliitaka kamati hiyo kuwatetea wanawake hasa wajane kumiliki ardhi baada ya kufiwa na waume zao.

Kafumbee alisema sheria nyingi za kimila zimekuwa zikitoa ardhi kwa wanaume au watoto wa kwanza wa kiume, lakini hazitoi ardhi kwa wajane na hata watoto wa kike hata kama wanakuwa wa kwanza kuzaliwa.

Alisema wakati wa ukoloni mfumo huo uliruhusu wanaume pekee kulimiki ardhi, lakini wanaliomba Bunge kupitia wabunge majimboni kusaidia kutoa elimu kwa viongozi wa kamati za vijiji kuwapa haki wajane na watoto wa kike katika kumiliki ardhi.

Ofisa Programu Mwandamizi kutoka HakiArdhi, Joseph Chombola alisema baadhi ya sheria zinatoa haki upande wa kiume wala si wanawake kuhodhi ardhi ya ukoo zinatakiwa kuendelea kupigiwa kelele ili kuondoka miongoni mwa jamii kwani binadamu wote wana haki ya kumiliki ardhi.

Alisema mila na desturi katika baadhi ya makabila zinapendelea wanaume na makabila machache kiasi cha asilimia 15 yanayoongozwa na wanawake ndiyo yanatoa nafasi kwa wanawake kusimamia ardhi.

Alisema hali hiyo pia inachangiwa na tamko la kimila la mwaka 1964 ambalo linampa haki mwanaume kumilikishwa ardhi na mwanamke kunyimwa. Akizungumza Mbunge wa Babati Mjini, Paulina Gekul (CCM) alisema hivi sasa watoto wa kike wanatakiwa kupewa haki ya kumiliki ardhi alisema atashangaa kuona familia za wasomi wa karne hii wanashindwa kuwaridhisha ardhi watoto wao wa kike.

Mbunge wa Korogwe Mjini, Timotheo Mnzava (CCM) alisema elimu inatakiwa kuendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali hasa katika ngazi za vijiji ambako mabaraza ya vijiji yamekuwa yakiwanyima haki wanawake pamoja na kuwapo wanawake wawakilishi.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shaban Shekilindi (CCM) alisema wao kama wabunge wamesikia ombi la asasi hizo na watalifanyia kazi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c0b273ec4cae4e51b0a24b44ceed8e79.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi