loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wabunge Kenya waja kujifunza uendeshaji mfuko wa Bunge

Wabunge Kenya waja kujifunza uendeshaji mfuko wa Bunge

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma ilipokea Sh milioni 68.5 kutoka Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Dodoma Mjini kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali jimboni humo.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya wabunge kutoka Kenya waliofika kujifunza kuhusu Uendeshaji wa Mfuko huo, Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Dodoma Mjini, Shaban Juma alisema fedha hizo ni za mwaka wa fedha 2018/19.

Juma ambaye ni mchumi wa jiji alisema, fedha za mfuko huo unaoongozwa na Mwenyekiti wake, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde zilitolewa kwa vikundi mbalimbali ambavyo vilitangaziwa katika kila kata kupeleka mradi itakayotekelezwa kwa mwaka huo.

Alisema kata 37 kati ya 41 zilizopeleka maombi na miradi inayopendekezwa ikiwemo ya ufugaji wa kuku na samaki kwa vikundi hivyo. Jumla ya vikundi 35 viliomba mradi wa ufugaji kuku na vikundi viwili viliomba mradi wa ufugaji samaki.

Juma alisema Kamati ya Mfuko wa Jimbo ilichambua maombi yote na kuazimia kuwa vikundi 35 vilivyoomba mradi wa kuku vipatiwe vifaranga 540 vya kuku aina ya kroiler pamoja na vyombo 16 vya maji, vyombo 16 vya vyakula na chanjo aina tatu, dawa na mifuko tisa ya chakula.

Kuhusu ufugaji wa samaki, vikundi viwili vilivyoomba mradi wa samaki, kamati iliridhia kuwa vipatiwe vifaranga vya samaki aina ya sato, matangi ya kuhifadhia maji na kufungwa mfumo wa maji kutoka kwenye samaki hadi kwenye mboga.

Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe alisema fedha za mfuko wa jimbo zinachechemua miradi midogo lakini vinataka pia halmashauri kutumia fedha za ndani kuongeza fedha katika miradi.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alisema pamoja na kwamba fedha hizo zinaletwa katika jimbo lakini zinakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) hata kama miradi inaibuliwa na wananchi wenyewe. Akizungumza kiongozi wa Wabunge kutoka Kenya, Fred Omondi alisema wamejifunza mengi kuhusu uendeshaji wa mfuko huo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7a577786b7f6b5dbc4b1816b21ff4d34.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi