loader
Dstv Habarileo  Mobile
Chai kuingiza dola milioni 102

Chai kuingiza dola milioni 102

RWANDA inatarajia kuingiza dola za Marekani milioni 102 (takribani Faranga bilioni 93) kutokana na kuuza chai nje ya nchi katika mwaka huu wa fedha, ikiwa ni zaidi ya Dola milioni 83 ilizopata mwaka jana.

Bodi ya Taifa ya Mazao ya Biashara Rwanda (NAEB) imesema ili kuingiza kiwango hicho cha fedha, nchi hiyo inatarajia kusafirisha nje ya nchi tani 34,000 za chai iliyosindikwa ikiwa ni zaidi ya tani 30,000 zilizosafirishwa mwaka jana.

Meneja wa kitengo cha bidhaa kutoka bodi hiyo, Issa Nkurunziza, alisema hayo wakati wa uzinduzi wa msimu wa chai kwa mwaka 2020. Aidha, alisema zaidi ya mbegu 88,000 za chai zinatarajiwa kupandwa katika mwaka huu wa fedha ili kuziba pengo la hekta 60 ambazo hazikupandwa katika wilaya ya Nyaruguru.

Alisema wanatarajia kutumia takribani tani 11,000 za mbolea katika mazao ya chai yaliyopandwa katika hekta 5,000 katika wilaya ya Nyaruguru na kufanya kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa wananchi.

Waziri wa Kilimo wa Rwanda, Gérardine Mukeshimana, alisema sekta ya chai nchini humo imezidi kukua kila mwaka, huku ikiendeshwa na viwanda vinne kikiwamo cha Nyabihu ambacho mwezi huu kimevunja rekodi kwa kuuza kilo moja ya chai Dola 7.22 za Marekani (sawa na faranga 6,624.89) katika soko la Mombasa Tea Auction.

Rwanda ina wakulima wa chai 42,000 na katika mwaka wa fedha uliopita asilimia 96 ya chai iliuzwa katika nchi 13 na soko kubwa likiwa Pakistan, Uingereza na Kazakhstan.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5bbce03da07d34b0b70d1075b119cb66.jpg

SERIKALI imetangaza kuwa watumishi wa umma kuanzia mwaka ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi