loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kilimanjaro Queens yatinga nusu fainali

KILIMANJARO Queens imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya michuano ya Wanawake ya CECAFA inayoendelea kwenye uwanja wa Chamazi Complex Dar es Salaam.

Hiyo inatokana na vipigo inavyoendelea kuvitoa katika kundi A, ambapo hadi sasa wameweza kushinda mechi zote mbili na kufunga mabao 13. Kilimanjaro Queens ambao ndiyo mabingwa mara mbili wa michuano hiyo, huu ni msimu wa tatu na kocha wake, Bakari Shime amepania kuhakikisha wanatwaa kwa mara ya tatu taji hilo ili kuweka rekodi ya kipekee kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Katika mchezo wa jana Kilimanjaro Queens iliingia kwa kuwashangaza wapinzani wao baada ya kocha Shime kubadilisha asilimia kubwa ya kikosi chake kilichocheza mechi ya kwanza dhidi ya Sudani Kusini na kuibuka na ushindi wa mabao 9-0, mmoja wao akiwemo nahodha Asha Rashid na Fatma Abdallah.

Mabao ya Kilimanjaro Queens katika mchezo wa jana dhidi ya Burundi yalifungwa na Donisia Daniel aliyefunga mabao mawili dakika ya 34 na 65, Asha Mwalala dakika ya 72 na Mwanahamisi Omary dakika ya 86.

Mbali na Kilimanjaro Queens timu nyingine inayofanya vizuri kwenye mashindano hayo ni timu ya taifa ya Uganda ambayo Jumapili iliibuka na ushindi wa mabao 13-0 dhidi ya Djibout na pengine inaweza kuwa timu inayoweza kutoa changamoto kwa timu yoyote kati ya zinazoshiriki mashindano hayo.

Uganda ambayo ipo kundi B, pamoja na mataifa ya Kenya, Ethiopia na Djibout ni miongoni mwa nchi ambazo imewahi kutolewa na Tanzania katika hatua ya nusu fainali mwaka 2016 jijini Kampala.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Kilimanjaro Queens, mambo sio mazuri kwa ndugu zao, Zanzibar Queens ambao walikubali kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Sudan Kusini ikiwa ni muendelezo wa matokeo mabaya kwa timu hiyo kwenye mashindano hayo kwani kwenye mchezo wao uliopita, walipokea kipigo kama hicho kutoka kwa timu ya taifa ya Burundi.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

1 Comments

  • avatar
    Zena Kashaga
    21/11/2019

    Ripoti Nzuri sana Mohamed , waandishi jitahidini pia kuhamasisha watanzania kuhudhulia uwanjani wachezaji wanahitaji sana support na inaimpact kubwa kama mlivyoona match zilizopita

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi