loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kwa nini uzee isiwe miaka 70?

PENGINE ni wakati wa kufi kiria tena jinsi tunavyopima na kufafanua uzee (nchini Uingereza) kwa sababu watu wengi sasa wanafi ka umri wa miaka 80 na zaidi wakiwa bado na nguvu na afya njema, wanasema wataalamu.

Timu ya maofisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (ONS) wanasema ingawa imezoeleka kwa muda mrefu kwamba miaka 65 ndio umri unaoelezwa kwamba ni mwanzo wa uzee, kwa sasa miaka 70 inaweza kuonekana mwanzo wa uzee badala ya 65.

Hiyo ni kwa sababu watu wengi ambao hufikisha umri wa miaka 65, bado wana matarajio ya kuishi miaka 15 mingine au zaidi.

Uzee ni umri gani?

Kwa kawaida miaka 65 ndio imekuwa ikichukuliwa kama mahali pa kuanzia uzee wa mtu kwa hapa Uingereza. Kwa miongo kadhaa umri huo umekuwa ndio rasmi wa kustaafu na hivyo mtu kuanza kuishi kwa pensheni ya serikali.

Lakini mifumo ya kufanya kazi inabadilika na umri wa pensheni unaongezeka kwa wanaume na wanawake - itafikia miaka 66 mwaka 2020 na 67 ifikapo 2028.

Timu ya ONS inasema kwa sasa kadri siku zinavyoongezeka watu wanaishi maisha marefu zaidi na yenye afya. Hiyo inamaanisha kwamba tunapaswa sasa kuzingatia miaka ambayo watu wanaweza kuishi kuanzia ile tunayowaita wazee na si vinginevyo.

Mabadiliko ya nyakati Kituo cha ONS, idara ya uzee na demografia iliangalia idadi ya watu, afya zao na umri wa kuishi kwa kulinganisha mwenendo wa wakati wa sasa na uliopita na kuona kwamba kuna haja ya kubadili mtazamo.

Ikiwa mtu unachukua kipimo cha wastani wa miaka 15 ya maisha yaliyobaki kwa Waingereza wengi baada ya kufikia uzee, basi umri wa wastani ambao mtu atapaswa kuonekana mzee umebadilika sana kuanzia karne iliyopita.

Mnamo mwaka 1951 ONS wanasema wanaume na wanawake wenye umri wa miaka 60 walitarajiwa kuishi wastani wa miaka 15 mingine.

Kufikia miaka ya 1990 hali ilikuwa imebadilika kuwa miaka 65 na kwa sasa umri huo umehamia miaka 70.

Kufikia mwaka 2057, wataalamu wanatabiri kwamba umri huu wa wastani wa uzee utapanda tena hadi 75 kwa maana ya mtu wa miaka 75 atakuwa anatarajia kuishia miaka 15 zaidi akiwa bado na afya njema.

Ongezeko la umri wa kuishi nchini Uingereza linaelezwa kwamba limetokana na maboresho katika huduma za afya na hali ya maisha.

Lakini mabadiliko ya kiafya kwa idadi ambayo mtu anatarajia kuishia baada ya kufikia umri wa uzee, yamekuwa pia yakipungua kwa baadhi ya watu na kuongezeka kwa baadhi ya wengine. Libby Webb, meneja mwandamizi wa utafiti huu uliohusu umri na mabadiliko ya nyakati anasema:

“Watu walio na umri wa miaka 70 sasa wana matarajio sawa ya maisha na afya sawa na watu wenye umri waliokuwa na miaka 65 miaka kadhaa huko nyuma. Tunaona watu wakiishi vizuri zaidi sasa kuliko vile walivyokuwa huko nyuma. Lakini anakiri kwamba bado wazee wengi hupitia kipindi kigumu cha afya mwisho mwisho wa maisha yao.

Anasema kutokana na kuboreka kwa umri wa kuishi inamaanisha pia kuwa sasa kuna wazee wengi pia wenye mahitaji mengi ya huduma za afya na kwamba bado hakuna usawa sana wa huduma za kiafya kati ya wazee matajiri na masikini. Lakini anasema hali ya jamii kuwa na wazee wengi (aging society) hakupaswi kuangaliwa kwa jicho hasi.

“Tunajua kuwa wazee hutoa michango muhimu kwa jamii yetu kwa mawazo yao ya busara na wanaopata pensheni au kujishughulisha bado hutoa pia mchango kwenye uchumi,” anasema.

Chanzo: Jarida la BBC

FIKIRIA tunda linaloweza kutumiwa kukuza uchumi, kutumiwa kama dawa, kiungo, ...

foto
Mwandishi: LONDON, Uingereza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi