loader
Picha

Taa barabarani zakuza uchumi Ruangwa

ZAIDI kilomita 9.04 za barabara mjini Ruangwa zimejengwa kwa kiwango cha lami.

Msaidizi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye masuala ya jimbo hilo, Fadhil Liwaka amesema mjini Ruangwa kuwa zimetengwa fedha za kujenga barabara kutoka Nanganga kwenda Ruangwa na itajengwa kwa kiwango cha lami.

Amesema kwenye kila barabara ya lami mjini humo kuna taa za barabarani na kwamba, kuna kilomita nane nyingine barabara zitawekwa taa kwenye maeneo ya miji jimboni humo ukiwemo wa Nanganga, Nandagala, Mbekenyela, Chienjele, na Mandawa.

“Sasa hivi ukipita usiku utaona watu wanachoma mahindi, watu wanauza maandazi, watu wanauza samaki, tunataka sasa hali ya uchumi na kasi ya kutafuta fedha iwe kubwa kupitia hizi jitihada hizi zinazofanywa na Serikali”amesema Liwaka.

Amesema, tofauti na miaka ya nyuma Ruangwa inafikika kwa urahisi kwa kuwa usafiri si tatizo tena, na kwamba, pia barabara kutoka Ruangwa kwenda Nachingwea imeshafanyiwa upembuzi yakinifu.

Amesema, barabara kutoka Ruangwa kwenda Kilanjelanje ikifunguka itakuwa muhimu kwa uchumi wa eneo hilo kwa kuwa itarahisisha usafiri wa kutoka Dar es Salaam na maeneo mengine nchini hivyo kasi ya maendeleo itaongezeka.

Liwaka ameyasema hayo wakati akizungumza na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuhusu utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015.

“Bado kuna haja ya kujenga kilomita tano nyingine ili kuweza kuwawezesha sasa wa Ruangwa wawe na uhakika wa kutembea ndani ya mji wao bila kupitia kwenye vumbi. Kwa hili limekwenda vizuri na barabara zote zinapitika” amesema.

Liwaka amesema, barabara za ndani zinazosimamiwa na TARURA (Wakala wa Barabara Vijijini) zimeunganishwa hivyo barabara kutoka kijiji kimoja hadi kingine zinapitika Kwa upande wa mawasiliano amesema, Ruangwa kuna usikivu mzuri wa mawasiliano kutokana na uwepo mitandao ya kampuni ya simu za mkononi.

“Kwa sasa hivi huwezi ukaenda sehemu ukakosa kuwasiliana, ni namna tu ya kuchagua mtandao gani unapatikana hapa, hizi ni juhudi ambazo zimefanywa na Mheshimiwa Mbunge lakini pia na Serikali ili kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa na mawasiliano ambayo ni nguzo muhimu sana katika kukuza uchumi na maendeleo” amesema Liwaka.

ILI kukabiliana na ugonjwa wa Covid- 19 unaosababishwa na virusi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi