loader
Picha

Betri za simu kutengenezwa Ruangwa

JIMBO la Ruangwa mkoani Lindi linajiandaa kupata kiwanda cha kutengeneza betri za simu.

Msaidizi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye masuala ya jimbo, Fadhil Liwaka amesema, kiwanda hicho kitapata malighafi wilayani humo hivyo kushawishi uwekezaji wa viwanda vya simu.

“Kwa hiyo ndio kusema kwamba kiwanda hiki cha kutengeneza betri za simu ambacho madini yake yanapatikana Ruangwa kikishaanzishwa tunakwenda kufungua sasa kwanza soko lakini la pili tunafungua viwanda vingine ambavyo sasa materials (malighafi) yake yanaendana na hizi betri zinazopatikana hapa Ruangwa” amesema Liwaka wakati akizungumza na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

“Tumekwishakutenga maeneo ya viwanda tayari, tunakaribisha wawekezaji na kwa wale wote ambao wapo tayari waje kufanya hiyo kazi” amesema.

Kwa mujibu wa Liwaka, malighafi kwa ajili ya viwanda si tatizo Ruangwa kwa sababu kuna madini mengi ikiwemo dhahabu, graphite, vito, chuma na shaba, tayari kuna migodi ya madini wilayani humo na uwekezaji kwa ujumla umefikia hatua nzuri.

“Lakini pia tunalo soko la madini, soko la mkoa lipo hapa kwa hiyo huduma zote za kimasoko zinazohusu madini zinapatikana hapa. Kwa hiyo wachimbaji wetu wana uhakika wa kuuza madini yao salama kabisa na kwa bei inayoridhisha kulingana na soko linavyohitaji” amesema Liwaka.

Amemshukuru Rais John Magufuli kuipa heshima Ruangwa kwa kukubali miradi mikubwa itekelezwe Ruangwa na kuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.

“Hatuna cha kumlipa ila wajibu wetu sisi ni kusimama bega kwa bega na yeye, kumuombea dua usiku na mchana lakini pia kumuunga mkono kila hatua anayokwenda, tunampenda sana na tuna imani nae” amesema Liwaka.

ILI kukabiliana na ugonjwa wa Covid- 19 unaosababishwa na virusi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi