loader
Picha

Wapongeza maboresho utoaji taarifa mtandao

MABORESHO makubwa ya utoaji taarifa za ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na kazi kwa mtandao ‘e-notifi cation’ yamepongezwa. Pongezi hizo zimetolewa na wadau baada ya mafunzo ya hivi karibuni kwa waajiri yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Mbeya.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dk Abdulsalaam Omar amesema mfuko umerahisisha upatikanaji wa huduma zake kwa mtandao na kuzisogeza karibu na wadau wake.

“Kwa sasa wadau wa mfuko wanaotumia huduma za mtandao hawalazimiki kufika kwenye ofisi zetu ili kupata huduma bali wanaweza kupata huduma hizo kutoka popote nchini, jambo lililopunguza gharama na kuokoa muda utakaotumika kuongeza uzalishaji kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa,”alisema.

Alisema mfuko umetoa fursa wateja kupata huduma kwa mifumo ya elektroniki (Tehama). Baadhi ya mifumo hiyo iliyosimikwa ni Mfumo wa Usajili ambao unamwezesha mwajiri kujisajili na kupata hati ya usajili papo hapo.

Mwingine ni wa uwasilishaji michango ambao unamwezesha mwajiri kutunza taarifa za wafanyakazi na kuwasilisha michango. Alisema michango huwasilishwa kupitia nambari ya udhibiti na kupata stakabadhi ya kielektroniki.

Mwingine ni wa uwasilishaji wa taarifa za tukio la ajali, ugonjwa na kifo. Alisema mfumo huo unamwezesha mwajiri kutoa taarifa ya tukio kwa wakati, kuwasilisha nyaraka na kujua hatua iliyofikiwa katika uchakataji wa madai kwa njia ya mtandao. Akizungumza katika mafunzo hayo, Meneja Tathmini za Vihatarishi Mahali pa Kazi wa WCF, Naanjela Msangi alitoa mwito kwa waajiri nchini kufanya tathmini ya viwango hatarishi kwa kadri inavyohitajika ili kuhakikisha usalama na afya za wafanyakazi vinazingatiwa.

Washiriki wa mafunzo hayo wamepongeza uwepo wa mifumo hiyo ya kielektroniki nchini kwani kutarahisisha uwasilishaji wa nyaraka. “Utaratibu wa kuwasilisha madai ya fidia kwa mtandao utapunguza gharama za uendeshaji,” alisema Sasilo Seif wa kampuni ya ujenzi China Geo Engineering Corporation, Kyela, Mbeya.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mbeya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi