loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwakinyo, Tinampey hapatoshi leo Uhuru

ILE siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi hapa nchini hatimaye leo imefi ka, ambapo kutakuwa na pambano la ngumi la kukata na shoka litakalowakutanisha bondia wa ngumi za kulipwa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo dhidi ya Arnel Tinampay wa Ufi lipino.

Pambano hilo la uzani wa Super Walter lisilo la ubingwa ni la raundi 10 litafanyijka katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Hili ni pambano la kwanza la kimataifa kwa Mwakinyo kucheza katika ardhi ya Tanzania, pambano lake la mwisho lilikuwa Machi mwaka huu nchini Kenya, ambapo alimshinda kwa ‘Technical Knock Out’ (TKO) mpinzani wake, Sergio Gonzalez kutoka Argentina.

Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo alisema kuwa alikuwa akilisubiri pambano hilo kwa muda mrefu na amejiandaa vizuri na ameahidi kumuangusha kwenye raundi za mwanzoni.

Alisema licha ya kukutana na bondia mwenye uwezo mkubwa kutokana na ukweli kwamba anatokea kwenye gym ya bondia mkubwa duniani, Manny Pacquiao lakini haoni cha kumtisha na kumnyima ushindi mbele yake.

“Tumejiridhisha kuwa Tinampaya ni bondia aliyekidhi vigezo vya kupambana na mimi na atanipa upinzani mkubwa, nimejiandaa vizuri kuhakikisha nashinda katika ardhi ya nyumbani ili kudhihirishia umma kuwa nipo vizuri na pia hiyo itakuwa ni chachu ya kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi hapa nchini,” alisema Mwakinyo.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi