loader
Picha

Amunike aomba kibarua Chipolopolo

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mnigeria Emmanuel Amunike ameomba kazi ya kufundisha timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’.

Ikumbukwe Amunike alifukuzwa kazi Tanzania baada ya kuwa na mwenendo mbaya ndani ya kikosi cha Stars, hasa pale ilipotolewa katika Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2019 nchini Misri katika hatua ya makundi.

Hivi karibuni, Amunike alihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, na kusema kuwa anatafuta kazi sababu mpaka sasa hana kibarua chochote. Maombi yake ya kazi kwenda Chipolopolo yameungana na makocha wengine ambao wameomba kazi ndani ya timu hiyo ambayo ni kongwe ndani ya barani Afrika.

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi