loader
Picha

Chadema yamaliza chaguzi za kanda

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema uchaguzi wa viongozi wa nafasi mbalimbali wakiwemo wenyeviti wa kanda zake zote umefanyika kwa kuzingatia misingi ya kidemokrasia kikiwa tayari kwa ajili ya uchaguzi ngazi ya Taifa unaotarajiwa kufanyika Desemba 18, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alisema uchaguzi huo uliomalizika jana kwa kanda za Serengeti, Nyasa, Unguja pamoja na Kanda ya Kati, umefanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu zake kama inavyofanyika wakati wote.

Makene alisema kufanyika kwa uchaguzi huo katika kanda hizo, kunakamilisha uchaguzi wa ngazi hizo katika kanda zake 10 ikizihusisha kanda zingine za Pwani, Kaskazini, Magharibi, Kusini, Pemba, Katavi, Serengeti na Victoria, ambazo nafasi zilizokuwa zikiwaniwa katika uchaguzi huo ni Mwenyekiti, Makamu na Mweka Hazina.

Miongoni mwa vishindo vya uchaguzi huo ni kuanguka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini, Cecil Mwambe, wawili ambao pia wamechukua fomu za kuwania uenyekiti wa Taifa dhidi ya Freeman Mbowe.

Juzi chama hicho kilifanya uchaguzi katika Kanda za Kaskazini na Kusini ambako kwa Kanda ya Kaskazini, Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema aliibuka na ushindi na kuwa Mwenyekiti wa kanda hiyo kwa kupata kura 78 akimbwaga mpinzani wake Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini aliyepata kura 23.

Uchaguzi huo ulifanyika jana mjini Arusha, pia ulishuhudia nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa kanda hiyo ikienda kwa Yosepha Komba aliyepata kura 76 na Mweka Hazina akiwa Anna Gideria aliyepata kura 68.

Kanda ya Kusini, Suleiman Mathew amefanikiwa kuwa Mwenyekiti mpya akimbwaga Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe ambaye hivi karibuni alitangaza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti Taifa wa Chadema.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imechukuliwa na Salum Barwan huku Mweka Hazina akiwa Mario Milinga.

Uchaguzi wa Kanda ya Pemba kura kwenye mabano, Mwenyekiti wa kanda hiyo ni Hafidhi Ali Saleh (27), Makamu Mwenyekiti Time Ali Suleiman (38) huku Mweka Hazina akiwa Ali Khamis Ali (29).

Kanda ya Victoria aliyeibuka kuwa Mwenyekiti ni Ezekia Wenje huku Kanda ya Pwani ikishuhudiwa aliyekuwa Mwenyekiti wa kanda hiyo ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akishindwa kutetea kiti chake baada kupigiwa kura 48 za hapana dhidi ya kura 28 zilizomkubali.

Kwa sasa matumaini ya Sumaye yamebaki katika ugombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa akitarajiwa kuchuana vikali na Mwenyekiti wa muda mrefu Mbowe pamoja na Mwambe.

Magnus Mahenge, kutoka Dodoma anaripoti kuwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini nchini, Lazaro Nyalandu ameibuka kidedea katika nafasi ya uenyekiti wa chama hicho baada ya kupata kura 60 (sawa na asilimia 66.8) kati ya 86 zilizopigwa katika uchaguzi huo.

Nyalandu alichaguliwa jana katika uchaguzi uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama hicho (Bavicha), Patrick Sosopi akusaidiana na Katibu Mkuu wake, Julius Mwita.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Sosopi alisema aliyekuwa mwenyekiti wa kanda hiyo, Alphonce Mbasa amepata kura 26 ( sawa na asilimia 33.2) uchaguzi huo.

Kwa nafasi ya Mweka Hazina, Mbunge wa Viti Maalumu, Devotha Minja aliibuka kidedea katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 44 sawa na asilimia 51.2 huku mshindani wake, Tully Kiwanga akipata kura 48.8.

Wakati huo huo, tukiwa tunaenda mitambo, habari zilizotufikia ni kwamba Ester Matiko alimgalagaza mgombea mwenzake, John Heche baada ya Matiko kupata kura 44 huku Heche akiambulia kura 38 kwa Kanda ya Kaskakazini.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi