loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kenya kutumia bil 13/- Olimpiki 2020

MKUTANO Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Kenya (Nock) umeidhinisha Sh milioni 600 za Kenya (sawa na Sh bilioni 13.5 za Tanzania) kwa ajili ya bajeti ya michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Rais wa Nock, Paul Tergat akielezea zaidi kuhusu bajeti hiyo alisema kuwa Sh milioni 250 za Kenya (sawa na Sh bilioni 5) zitaenda katika maandalizi na kufuzu kwa ajili ya michezo hiyo ya Olimpiki ya majira ya joto itakayofanyika kuanzia Julai 24 hadi Agosti 9 katika mji huo mkuu wa Japan.

Mpango wa Nock inakadiria Kenya itapeleka wawakilishi takribani 100 katika michezo hiyo ya Olimpiki ya Tokyo. Kenya iliwakilishwa na wachezaji 89 wakiwemo wanaume 47 na wanawake 42 katika michezo ya Olimpiki ya Rio 2016, Sh bilioni 12.

"Bado tuna timu ambazo zinajaribu kufuzu kwa ajili ya kushiriki michezo hiyo, ambayo itafanyika katika miezi minne ya mwanzo ya mwaka ujao,” alisema Tergat, wakati akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa mwaka kwenye hoteli ya Panari, Nairobi mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya michezo ambayo bado haijakamilika kufuzu kwake, ambayo itafanyika mwakani ni pamoja na ngumi, mpira wa wavu kwa wanawake, meza, judo, tae kwon-do na mieleka.

Tayari karibu wachezaji 46 wamefuzu kwa ajili ya michezo hiyo ya Olimpiki wakiwemo wanariadha 28, waogeleaji wawili na mchezo wa rugby wa wachezaji saba kwa saba kwa wanaume na wanawake. Tergat alisema kuwa sasa wataihusisha serikali mara moha ili maandalizi yaweze kuendelea…

Tergat alithibitisha kuwa Jiji la Kurume huko Fukuoka, Japan ndio timu ya Kenya itapiga kambi kablaya michezo hiyo, lakini alibainisha kuwa kambi ya timu hiyo hapa nyumbani itatangazwa baadae.

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi