loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Logarusic ataka kurejea Simba

KOCHA wa zamani wa Gor Mahia na AFC Leopards, Zdravko Logarusic (pichani chini) amehusishwa na kutaka kurudi tena Simba ya Tanzania baada ya klabu hiyo kummwaga kocha wake, Mbelgiji Patrick Aussems.

Simba kwa sasa inasaka kocha baada ya kuachana na Mbelgiji huyo, ambaye anatuhumiwa kushindwa kuiwezesha timu hiyo kuwa na kiwango kizuri na wachezaji kutokuwa na nidhamu.

Kocha huyo Mcroatia anaweza kurudi tena Simba, ambayo aliwahi kuifundisha katika msimu wa mwaka 2013/14. Logarusic mwishoni mwa wiki iliyopita alitimuliwa kutoka katika timu ya taifa ya Sudan baada ya kushindwa kuiongoza timu hiyo kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019 Misri) na ile ya Chan 2020 nchini Cameroon.

Mfaransa Didier Gomes pia inaelezwa kuwa naye anatajwa kuziba pengo hilo la ukocha Simba. Mafanikio ya Gomes ni pamoja na kuiongoza klabu ya Rwanda ya Rayon Sport kutwaa taji la Ligi Kuu na timu ya Cameroon ya Coton Sport katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Pia aliiongoza timu ya Guinea ya Horoya, ambayo iliongoza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa mwaka 2019/20. Simba, ambayo ni ‘nyumbani’ kwa nyota wawili wa zamani wa Gor Mahia, Meddie Kagere na Francis Kahata kwa sasa inaoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kucheza raundi 10.

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi