loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bao la Messi laibeba Barcelona

LIONEL Messi (pichani) alifunga dakika za mwisho bao safi la ushindi wakati mabingwa wa Hispania, Barcelona wakiichapa Atletico Madrid kwa bao 1-0 na kurejea kileleni mwa La Liga juzi.

Messi alifunga bao safi akiwa ndani ya eneo la penalti zikiwa zimebaki dakika nne kabla ya mchezo huo kumalizika likiwa ni bao lake la 11 katika mechi 10 msimu huu. Juhudi za kipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen mara mbili zilizuia jitihada za kufunga za Mario Hermoso na Alvaro Morata na kuikosesha Atletico Madrid mabao ya kuongoza.

Ushindi huo unaifanya Barcelona kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi kileleni ikiwa juu ya Real Madrid kwa tofauti ya mabao. Real Madrid ya Zinedine Zidane iliifunga Alaves 2-1 na kupanda juu Jumamosi, wakati Sevilla ikiwa nyuma kwa pointi moja, iliifunga Leganes 1-0 katika mchezo ulioiweka timu hiyo kwa muda katika nafasi ya pili Jumapili.

Atletico ilikosa nafasi kibao na kama ingefunga ingekuwa mbele, lakini mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani, Ter Stegen aliokoa shuti kali la karibu la Hermoso na baadae mpira wa kichwa wa Morata na kufanya kikosi cha kocha Diego Simeone kushindwa kupata bao.

Kipigo hicho kinaifanya kikosi hicho cha kocha Simeone, ambao ni mabingwa wa msimu wa mwaka 2013-14 kimejikuta pointi sita nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Hispania.

S IKU 414 baada kuanza kwa msimu wa Ligi ya ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi