loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ndalichako apongeza Kanisa Katoliki huduma ya elimu, afya

KANISA Katoliki limeonekana kuendelea kuikosha Serikali kwa kuzidi kuwa na mchango mzuri katika utoaji huduma kwenye sekta za elimu na afya.

Kati ya mambo ambayo yanaonekana kufurahiwa na serikali ni pamoja wa kupikwa vizuri kwa wahitimu katika shule na vyuo vinavyomilikiwa na kanisa hilo, jambo ambalo limetajwa kuwapa uwanja mpana kwenye mapambano ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alielezea msimamo wa serikali kwenye Mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Saint Agustine (SAUT), Kampasi ya Mbeya ambapo jumla ya wahitimu 650 walitunukiwa Shahada, Stashahada, Astashahada na cheti cha awali katika nyanja mbalimbali za kitaaluma, kati yao wakiwemo wanaume 366 na wanawake 284.

Katika mahafali hayo, Profesa Ndalichako alisema elimu inayotolewa na shule za Kanisa Katoliki haitii shaka kuwa wahitimu wanapikwa ipasavyo na ndiyo sababu wanapomaliza masomo yao wamekuwa sehemu ya Watanzania wenye uwezo mkubwa kiutendaji.

“Serikali inatambua mchango wa kanisa hili hasa katika uwekezaji kwenye sekta za elimu na afya. Hebu tujiulize kama tawi hili la Sauti Mbeya lisingekuwepo kundi hili la wahitimu hawa lingekuwa wapi leo hii kama siyo mtaani? Tunahitaji muendelee na jitihada hizi za kushirikiana na serikali kwa kuwa mkisema muiachie peke yake inaweza kuchelewa kutokana na kuwa na mambo mengi,”alisisitiza.

Waziri huyo aliwasihi wahitimu wote kwenda kuitendea haki elimu waliyoipata kwa kuchapa kazi kwa bidii, maarifa na weledi wakitambua kufanya hivyo watakuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza chuo hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila aliwataka wahitimu kutambua kuwa wengi wa vijana wanaolalamika ukosefu wa ajira mitaani wamejikita katika kuzisubiri badala ya kuzitafuta.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Mbeya

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi