loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CCTV zaumbua washirikina Mji Mkongwe

MATUKIO ya kishirikina ikiwemo wananchi kuvunja nazi kama kafara katika maeneo ya njia panda Mji Mkongwe yametajwa kuongoza na kurekodiwa kwa wingi katika kamera za CCTV zilizowekwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Unguja.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Shamata Shaame Khamis wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua kamera za CCTV zilizowekwa katika eneo la Mji Mkongwe kwa kiasi gani zimefanikiwa kuwanasa wahalifu.

Khamis alisema hadi sasa kamera hizo hazijafanikiwa kuwanasa wahalifu wanaovunja sheria au wahalifu katika eneo la Mji Mkongwe na maeneo ya jirani. Alisema kamera hizo hadi sasa zimefanikiwa kuwamulika watu wanaofanya vitendo vya kishirikina kwa kufanya kafara ya kuvunja nazi na matikiti maji katika maeneo ya njia panda zilizopo Mji Mkongwe.

Alisema eneo la njia panda katika Hospitali ya Mnazi Mmoja pamoja na barabara ya jirani na makazi ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi yamekuwa yakitumiwa na watu wenye imani za kishirikika kwa kuvunja nazi na matikiti maji.

“Kamera zetu hadi sasa hazijafanikiwa kuwanasa wahalifu isipokuwa matukio ya kishirikina na kafara kwa kuvunja nazi nyakati za usiku yamerikodiwa, tunafanya uchunguzi na wahusika tutawachukulia hatua,” alisema.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka kamera za CCTV katika maeneo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar pamoja na maeneo ya jirani kwa ajili ya kudhibiti matukio ya uhalifu.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi