loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shule ya Zamzam kuwajengea yatima madarasa manne

KATIKA kuboresha na kuinua kiwango cha ufaulu, Shule ya Msingi ya Kiislamu ya Zamzam jijini Dodoma ina mpango wa kujenga madarasa manne, yatakayowezesha watoto wa mazingira magumu kutoka mikoa mbalimbali nchini, kupata fursa ya kusoma.

Akizungumza wakati wa mahojiano, Mkurugenzi wa Dalai Islamic Centre, Rashidi Bura alisema miongoni mwa mikakati waliyoiweka ni kujenga mabweni manne ili kuweza kupokea watoto kutoka mikoa mbalimbali kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Alisema fedha za ujenzi wanategemea kuzipata kupitia michango mbalimbali na wahisani.

“Mkakati wetu ni kuhakikisha tunalea watoto katika maadili ya hali ya juu ambayo yatawasaidia kwa siku za usoni kuwa rai wema watakaolitumikia taifa kwa moyo,”alisema.

Pia, alisema sasa wanajenga madarasa manne, ofisi mbili za walimu na matundu 20 ya vyoo, ikiwemo vyoo viwili kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu. Alisema kwa sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 350 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Kati yao kuna watoto 90 ambao ni yatima na wale wanaotoka katika mazingira magumu, wanaosoma bila kulipia gharama zozote.

Alisema wanafunzi wa shule hiyo, wamekuwa wakilipa ada Sh 400,000 kwa mwaka na chakula kimekuwa kikitolewa bure kwa watoto wote. Alisema shule hiyo ina uwezo wa kuchukua watoto 600 na sasa wanapokea maombi mapya na watachagua wanafunzi kulingana na idadi ya madarasa yaliyopo.

Bura alitaja matatizo yao ni upungufu wa madarasa, mabweni sehemu ya kuabudia na uzio. Alisema malengo ya baadae ni kuanzisha shule ya sekondari ili wanafunzi wanapomaliza darasa la saba,waendelee na sekondari hapo.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi