loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

14 wauawa katika shambulizi kanisani

WATU 14 wameuawa baada ya kutokea shambulizi la wazi ndani ya Kanisa nchini Burkina Faso. Waathirika wa shambulizi hilo la siku ya Jumapili, walikuwa wakisali katika Kanisa la Hantoukoura, Mashariki mwa nchi hiyo.

Watu waliofyatua risasi hizo, bado hawajafahamika na hata lengo lao bado halijawekwa wazi. Mamia ya watu wameuawa katika taifa hilo katika miaka ya hivi karibuni na kundi la kigaidi la Jihadist.

Wameuawa kutokana na mvutano wa kikabila na kidini, hasa katika mpaka wa Mali. Taarifa kutoka serikalini zinasema pamoja na watu hao kuuawa, idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa kutokana na tukio hilo.

Idara ya usalama nchini humo, ilibainisha kuwa watu wenye silaha ndio wamefanya shambulio hilo. Chanzo kingine cha habari kimesema kuwa wanaume hao wenye silaha walitumia pikipiki.

Oktoba mwaka huu watu 15 waliuawa na wawili walijeruhiwa vibaya katika shambulizi lililotokea katika msikiti. Mashambulizi ya kigaidi yameongezeka nchini Burkina Faso tangu mwaka 2015 na yamesababisha maelfu ya shule kufungwa.

Mgogoro kati ya nchi hiyo na nchi jirani ya Mali, umekuwepo tangu mwaka 2012, baada ya wanamgambo wa Kiislamu kuchukua eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo, kabla ya jeshi la Ufaransa kuwaondoa.

foto
Mwandishi: OUADADOUGOU, Burkina Faso

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi