loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yaliyomo ndani ya ripoti ya BBI

WIKI iliyopita, Rais Uhuru Kenyatta alizindua ripoti ya tume ya maridhiano inayotarajiwa kupigiwa kura ya maoni na na wananchi na hatimaye kuidhinishwa na Bunge kuanza kutumika ili kuleta utengamano katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Miongoni mwa mambo yaliyoguswa katika ripoti hiyo, mfumo wa utawala, ambapo imependekeza kuwa Kenya iwe ikiongozwa na Rais ambaye ataitumikia katika kipindi cha miaka saba badala ya mitano.

Vilevile ripoti hiyo inampa Rais jukumu la kumchagua Waziri Mkuu kutoka chama chenye viti vingi bungeni ama muungano mkubwa bungeni, ambaye atachukua nafasi hiyo baada ya kuidhinishwa na Bunge.

Hata hivyo, nafasi ya Waziri Mkuu haitakuwa haina mamlaka mengi, kwani Rais anaweza akamfuta kazi wakati wowote, ingawa ndiyo atakuwa msimamizi mkuu wa kazi za kila siku za serikali.

Pia Waziri Mkuu anaweza akaondolewa kupitia kura ya kutokuwa na imani naye kwenye Bunge. Jopo la Maridhiano lilibuni nafasi hiyo kwa lengo la kumtuliza mshindi wa pili kwenye uchaguzi wa Rais na kuzuia ghasia za baada ya uchaguzi ambazo katika miaka ya karibuni zimekuwa zikitokea kila uchaguzi mkuu unapofanyika nchini humo.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema maeneo mengi ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi