loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakiuka taratibu za uchaguzi waonywa

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Burundi (CENI), Claver Kazihise, amezitaka mahakama kuwachukulia hatua wanaovunja sheria wakati wa uchaguzi.

Amewataka maofisa wa mahakama kuzijua taratibu na kanuni za uchaguzi zilizopo kwenye vifungu vya sheria ikiwamo adhabu kwa watakaoleta vurugu wakati wa uchaguzi.

Alisema hayo wakati wa semina maalumu ya maofisa wa mahakama iliyoandaliwa na CENI, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajia kufanyika mwakani.

Kazihise alisema kuna makosa mbalimbali yanayofanywa kwenye mchakato wa uchaguzi na kutoa mfano baadhi ya watu kupiga kura bila kuwa na haki ya kufanya hivyo na kupiga kura mara mbili katika uchaguzi mmoja.

Alisema katika makosa hayo, mpigakura anapewa adhabu ya kufungwa jela kwa siku 15 hadi miezi mitatu au kupigwa faini ya faranga za Burundi 200,000 au Faranga milioni moja.

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi