loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rwanda kupoza makali ya VVU kwa sindano

RWANDA ni moja ya nchi zitakazofanyiwa majaribio ya wagonjwa wa Ukimwi kuchomwa sindano badala ya kumeza vidonge vya ARVs kila siku.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Tiba Rwanda (RBC), Dk Sabin Nsanzimana, juzi alisema sindano hizo ni bora na njia endelevu katika matibabu hayo.

Alisema kwa kawaida vidonge vya ARVs vinamezwa kila siku, lakini sindano itakuwa ikidumu kwa wiki nane, ikiwa ni moja ya sayansi iliyobobea katika mkakati wa kumaliza Ukimwi duniani ambao ni ajenda ya mkutano wa 20 wa kimataifa wa kupambana na maambukizi ya VVU utakaofanyika Kigali wiki hii.

Katika mkutano huo zaidi ya watu 10,000 kutoka nchi 150 watakutana kujadili njia bora za kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi katika bara la Afrika lenye watu wengi walioathirika na ugonjwa huo.

Takwimu za mara ya mwisho kutoka RBC zinaonesha kuwa, kiwango cha ugonjwa huo Rwanda kimepungua kwa watu 26,000 wenye umri wa miaka 15 hadi 64 ambao wanaishi na ugonjwa huo, huku maambukizi mapya ya VVU yakiwa watu 5,400 kila mwaka.

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi