loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maboresho miundombinu kuvutia watalii Iringa

MABORESHO ya miundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yanayotarajiwa kuanza karibuni kupitia Mradi wa Kuendeleza Utalii Ukanda wa Kusini (REGROW) yatawezesha watalii kufi ka hifadhini kupitia mikoa ya Mbeya na Dodoma.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964, hifadhi hiyo kubwa kuliko zote nchini sasa imekuwa ikiingilika kupitia lango pekee lililoko Iringa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa vifaa kazi vya mradi huo wa REGROW uliofanyika katika hifadhi hiyo juzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda amesema maboresho hayo yatavutia idadi kubwa ya watalii kuitembelea wakiwemo wa ndani.

Kupitia maboresho hayo, Katibu Mkuu amesema serikali inatarajia yatainua mapato ya hifadhi hiyo, hatua itakayoiwezesha ijiendeshe kwa faida na kufikia hatua ya kutoa gawio serikalini.

Alisema hifadhi inajiendesha kwa kutegemea mapato ya hifadhi za Kaskazini kwani haijawa na watalii wa kutosha kuiwezesha kujiendesha.

“Sababu ni changamoto ya miundombinu ambayo ni kikwazo watalii kufika kuitembelea,” alisema na kutaja baadhi ya hifadhi nyingine nchini zenye changamoto kama hiyo.

Kupitia REGROW, Profesa Mkenda amesema wizara imejipanga kuboresha miundombinu ya hifadhi hiyo sambamba na kuitangaza ili kuhamasisha watalii wengi zaidi kuitembelea.

Amesema kupitia REGROW itajengwa miundombinu itakayowezesha watalii kuingia katika hifadhi kupitia mikoa ya Mbeya na Dodoma bila kusafiri hadi mkoani Iringa.

Amesema ujenzi wa barabara hizo utaenda na ujenzi wa madaraja katika maeneo mbalimbali ya hifadhi ili kuwawezesha watalii kuingia na kutoka katika hifadhi hiyo kwa urahisi zaidi.

Pamoja na maboresho hayo, Profesa Mkenda amesema wizara inatafakari kuanzisha utalii wa fukwe kuwapata pia watalii wa aina hiyo ambao hutumia meli kufanya utalii katika fukwe.

Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA ) Kanda ya Kusini, Dk Christopher Timbuka alisema REGROW itaboresha mazingira ya ujenzi wa maeneo ya kulaza watalii kuongeza idadi ya vitanda vya kulaza watalii ndani ya hifadhi.

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi