loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kufungwa benki Mbinga kwaathiri wakulima

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amesema kufungwa kwa Benki ya Wananchi ya Mbinga mkoani humo kumeathiri kiasi kikubwa uchumi wa wakulima na jamii.

Mndeme amesema hayo jana kwenye ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya mkoa wa Ruvuma (RCC) mjini Songea.

Amesema kufungwa benki hiyo kumesababisha baadhi ya wakulima kutomudu gharama za uendeshaji kilimo kwa kukosa mikopo ya pembejeo za kilimo iliyokuwa ikitolewa nao.

Alisema ili kukabiliana na hilo, serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya walioifilisi benki hiyo na kuikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi.

Mkuu wa mkoa alihimiza wataalamu kuzitumia mvua zilizoanza kunyesha mkoani humo kwa ajili ya kwenda kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima vijijini, badala ya kukaa ofisini tu.

Ametoa onyo kwa mawakala ambao watauza pembejeo za kilimo kwa bei kubwa tofauti na bei elekezi ya serikali.

Alisema atakayeenda kinyume atachukuliwa hatua kali za kisheria. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amesema migogoro kati ya wakulima na wafugaji inazidi kuongezeka hivyo ameshauri kujengwa kwa majosho na kutengwa kwa matumizi bora ya ardhi kubaini mae

UBALOZI wa Tanzania nchini China umetangaza kuwa kampuni ya Shandong ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Songea

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi