loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanesco kuwezesha Tanzania ya viwanda

MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk Alexander Kyaruzi amesema bodi hiyo itatoa ushirikiano wa asilimia 100 kwa shirika hilo katika kutekeleza miradi ya kimkakati ya umeme ambayo itachangia kufikia Tanzania ya viwanda na hatimaye kufanya biashara ya umeme.

Dk Kyaruzi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kutembelea miradi ya kimkakati wa kujenga njia kuu ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 na upanuzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Zuzu.

Alisema kwa sasa kazi inayofanyika ni kutekeleza miradi ya kuongeza uzalishaji wa umeme, kuboresha na kujenga njia kuu za kusafirisha umeme na miradi ya kusambaza umeme.

Bodi alisema inaisaidia Tanesco kutekeleza vipaumbele vya taifa vya kuhakikisha nchi inakuwa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda ambao unatengemea uwepo wa nishati ya umeme ya kutosha.

Kuhusu kusambaza umeme, Dk Kyaruzi alisema kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita yamefanyika marekebisho ya usambazaji umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro na kuwa juhudi hizo zimeelekezwa katika mikoa mingine ili kupunguza wasiwasi wa umeme kukatika katika.

Kuhusu maendeleo ya upanuzi wa Kituo cha Zuzu, Dk Kyaruzi alionesha kufurahishwa na hatua iliyofikia na kuwa kukamilika kwake kutasaidia Jiji la Dodoma kuwa na umeme wa uhakika.

Naye Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa njia kuu ya kilovolti 400 kwa ajili ya kuunganisha mfumo wa Gridi ya Taifa na zile za Kenya kwa upande wa Kaskazini na Zambia kwa upande wa Kusini, Peter Kigadye alisema hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo ni kujenga vituo vinne vya kupoozea umeme wa kilovolti 400.

Alisema vituo hivyo ni Dodoma, Singida, Sinyanga na Iringa ambavyo vitagharimu dola za

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi