loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Treni ya abiria Dar – Moshi kuanza rasmi leo

TRENI ya kwanza ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) inatarajiwa kuanza kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali kwenda mikoa ya Tanga na Kilimajaro leo, ikiwa ni baada ya kukamilika kwa taratibu mbalimbali za usafi ri huo ikiwemo majaribio ya njia ya safari.

Hatua hiyo inatarajiwa kuamsha matumaini mapya ya usafiri kwa wakazi wa mikoa ya kaskazini ambao wengi wao hujikuta wakipata adha kubwa ya usafiri hasa inapofika msimu kama huu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema tayari maandalizi ya safari hiyo inayotarajiwa kuanza saa 10 jioni yameshakamilika na kuwataka abiria wote wanaotarajiwa kusafiri na treni hiyo kuakikisha wanazingatia muda uliopangwa. Treni hiyo itakuwa inatoka Dar es Salaam kila Jumanne na Ijumaa na kutoka Moshi itakuwa kila Jumatano na Jumamosi kuanzia saa 10 jioni na kufika kituo husika saa 2 asubuhi.

Hata hivyo, Kadogosa hakuweka wazi idadi ya abiria waliokata tiketi kwa ajili ya safari hiyo ya kwanza kwa madai kuwa kwa muda huo alikuwa nje ya ofisi hivyo kukosa takwimu sahihi za abiria waliokwisha kukata tiketi zao, lakini alisisitiza kuwa waliokata tiketi ni wengi tayari kwa ajili ya kupokea huduma hiyo.

Awali TRC ilitangaza nauli za treni hiyo itakayopita Korogwe mkoani Tanga kuwa kuanzia Dar es Salaam hadi Korogwe nauli kwa daraja la tatu itakuwa Sh 10,700, daraja la pili kukaa Sh 15,300 na daraja la pili kulala ni Sh 25,400.

Aidha, kutoka Dar es Salaam hadi Moshi daraja la tatu ni Sh 16,500, daraja la pili kukaa Sh 23,500 na daraja la pili kulala Sh 39,100 ambapo kwa mujibu wa Shirika hilo, treni hiyo inatarajiwa kuwa na mabehewa tisa likiwemo moja kwa ajili ya kubebea mizigo.

Akizungumzia majabirio yaliofanywa kwa treni hiyo kwenda Moshi wiki iliyopita, Kadogosa alisema yalikwenda vizuri na kwamba kwa tathimini walioifanya treni hiyo ipo vizuri na hakukuwa na shida yoyote katika safari nzima.

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi