loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania bingwa Copa U-16 Mataifa ya Afrika

TIMU ya soka ya vijana ya Tanzania imeiadhibu Zimbabwe kwa mabao 6-2 katika mchezo wa fainali za mashindano ya kwanza ya COPA Coca-Cola kwa vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Mataifa ya Afrika na kutwaa ubingwa.

Tanzania ilionesha kiwango cha juu na kuibuka mshindi katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye viwanja vya MPESA Foundation Academy mjini Thika, Kenya jana. Taarifa kutoka Kenya zinasema kwamba mshindi wa kiatu cha dhahabu, Paul Nyerere alifunga mabao 3 ‘hat trick’ katika kipindi cha kwanza wakati wa fainali hiyo. Nyerere ameibuka mfungaji bora baada ya kufikisha mabao 7 kwenye michuano hiyo.

Mabao mengine yaliwekwa kimiani na Ndile Haruni, Rai Mohambi, Boniface Raphael na kuiwezesha Tanzania kutwaa taji la mabingwa wa Kombe la COPA Coca- Cola Afrika 2019.

Akizungumza mara baada ya mashindo hayo kuisha, Kocha wa Tanzania, Alex Mtweve alisema, timu yake ilistahili taji hilo.

“Tuliutawala mchezo tangu mwanzo na vijana wangu walionyesha ujuzi, kwa kweli tulikuja kwenye mashindano haya na lengo la kutwaa ubingwa, nashukuru vijana hawajaniangusha.”

Mtweve aliongeza kuwa siri ya ushindi wake imekuwa ni kucheza mchezo wa kushtukiza na kushambulia kwa nguvu. Mlinzi wa timu ya Tanzania, Chuma Ramadhan alifanya kazi kubwa pia ya kuiwezesha timu yake kutawala mchezo baada ya kuokoa hatari kadhaa golini kwake na kuzuia penalti moja wakati wa mchezo huo wa fainali.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chama ambaye alishuhudia fainali hiyo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana hao na kuwatakia kila la heri.

JUMLA ya mapambano 10 ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi