loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zanzibar yapania kufanya makubwa Cecafa

KOCHA wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Hemed Morocco amesema kuwa anakiamini kikosi chake kwa namna alivyokiona katika kuelekea kwenye michuano ya Cecafa Chalenji inayotarajia kuanza rasmi kesho Jumamosi.

Michuano hiyo safari hii inafanyika mjini Kampala nchini Uganda huku bingwa mtetezi ikiwa ni Kenya iliyotwaa kombe hilo mwaka 2017 kwa kuifunga Zanzibar katika fainali iliyoisha kwa sare 2-2 kabla ya kuibuka kidedea kwa penalti 3-2.

Morocco ameeleza kuwa kikosi chake ni kipana mno na kilikuwa na changamoto kubwa katika uteuzi wa wachezaji watakaoenda kuiwakilisha Zanzibar katika michuano hiyo. Pamoja na hayo, kocha huyo ameeleza kuwa kamili katika kila idara isipokuwa amekuwa na upungufu ambao ni wa muda mrefu katika nafasi ya beki wa kulia ingawa safari hii imeleta ahueni kutokana na kuwa na machaguo mengi katika nafasi hiyo.

“Changamoto ya kutaja kikosi ilikuwa kubwa, kikosi ni kizuri kila mmoja anajitoa isipokuwa katika nafasi ya beki wa kulia tangu mwaka 2017 imekuwa ikisumbua japokuwa safari hii nilikuwa na machanguo matatu kabla ya kuwachukua wawili ambao kulingana na mfumo, wote walikuwa wanaonesha uwezo mkubwa.

KLABU ya Yanga imetangaza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi