loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sudan Kusini, Ethiopia nje Cecafa

UONGOZI wa Baraza la Vyama vya soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeziondoa timu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia na Sudan Kusini kwa sababu hawakuweza kutekeleza majukumu yaliyopitishwa na mkutano wa makubaliano wa CECAFA uliofanyika Addis Ababa mapema mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicolas Musonye alisema moja ya majukumu hayo ni kulipa ada ya uanachama ambayo kila nchi inayoshiriki mashindano hayo inapaswa kutoa ambapo alisema ni Dola za Marekani 20,000 kwa kila nchi.

“Tulikubaliana kwa kila nchi shiriki kulipa kwa wakati ada ya uanachama kiasi cha Dola za Marekani 20,000; wameshindwa kutekeleza hilo na hivyo tumeamua kuwaondoa kwenye mashindano ya mwaka huu,”alisema Musonye.

Aidha, Musonye alisema mashindano ya Cecafa kwa upande wa wanaume yanatarajiwa kuanza kesho hadi Desemba 19 Kampala, Uganda na yale ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 yataanza Desemba 9 hadi 19 katika Viwanja vya FUFA Technical Centre, Njeru.

Alisema timu za wanaume ni tisa na zimepangwa katika makundi mawili ambapo kundi A lina timu za Uganda, Burundi, Somalia, Eritrea na Djibouti na Kundi B linaundwa na timu za Kenya, Tanzania, Zanzibar na Sudan.

Kwa upande wa timu za wanaume Tanzania Bara itafungua dimba kesho kutwa kwa kucheza na Kenya saa 10:00 na Zanzibar itaivaa Sudan, mchezo ambao utachezwa mchana. Desemba 10, Tanzania Bara itamenyana na Zanzibar na Sudan itaivaa Kenya na Desemba 14 Kenya itacheza na Zanzibar na Tanzania Bara itakutana na Sudan.

Alisema timu za Djibouti, Zanzibar, Tanzania Bara zilikuwa zimewasili Uganda na nyingine zilitarajiwa kuwasili muda wowote kabla ya mashindano kuanza. Pia Musonye alisema timu za wanawake ambazo zitashiriki ni wenyeji Uganda, Tanzania Bara, Uganda, Eritrea, Burundi, Kenya na Djibouti. Alisema mechi zote za wanaume zitaonenyeshwa

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi